Thursday, March 27, 2014

SERIKALI YATOA AMRI YA PIGA "RISASI HADI UUE"




SERIKALI imewaamrisha maafisa wa polisi kuwapiga risasi na kuwauwa washukiwa wa ujambazi waliowamiminia risasi waumini waliokuwa kanisani siku ya Jumapili na kuwauwa watu sita huku wengine 17 wakiachwa na mejeraha ya risasi.
Wakati huo huo polisi wametakiwa kuwauwa majambazi wanaoendelea kuhangaisha wakazi wa kaunti ya Mombasa.

Akitoa amri hiyo mwneyekiti wa kamati ya usalama katika kaunti ya Mombasa Bw Nelson Marwa alisema majangili na magaidi hawafai msamaha, huruma ama kupelekwa mahakamani huku akivitaka vyombo vya usalama kukabiliana nao mara moja.

Akiongea kwneye mkutano wa kiusalama kati ya viongozi wa makanisa yote katika kaunti hiyo kamishna huyu wa kaunti ya Mombasa alisema wahalifu waliouwa wamunimi kanisani hawafai kupelekwa mahakamani kwa kuua.

“Hao si watu wakutiwa mbaroni ati kwa sababu wamejihami! Wanafaa kumalizwa papo hapo. Kwa nini wapelekwe mahakamani ilhali wameuwa watu sita? Kuna haki gani kwa waliouwawa? Nani atakuwa shahidi yako kortini? Nani atawafufua uliowauwa ili wawe mashahidi wako? Lazima tuwe watu wa haki wakipatikana wauliwe maramoja” akaagiza.

Alisema operesheni ya kuwasaka wahalifu hao imesambazwa hadi kaunti za KIlifi na Kwale huku akionywa kwamba wataingia hadi katika Kaya kuwasaka.

Alisema kwa sasa wamekamata washukiwa 109 ambao wamo mikononi mwa maafisa wa polisi huku akiongeza kuwa hata kivukio cha feri kimezungukwa na maafisa wa polisi wenye mavazi ya sare na wale wenye mavazi ya kawaida.

“Kivukio cha Feri inayotumiwa na maelfu ya Wakenya huko tumetuma maafisa wa polisi washike doria. Wahalifu ambao wametorokea katika Kaya wajue tutawafuata hadi huko ndani serikali itafanya kile liwezavyo ili wachukuliwe hatua” akasema.

Mwenyekiti wa muungano wa makanisa Mombasa Askofu Wilred Lai alisema, “Wale ambao wanadhania watatutishia Kanisani wajue hilo ni ndoto Mkristo hawezi kutishika na kushindwa kwenda Kanisani. Tutaendelea kuhubiri amani na neon la Munguna atapambana na nyinyi.”
Walisema watawasaidia familia za wendazake na walioathirika kwa shambulizi la Kanisani ikiwemo mazishi.

Bw Marwa alisema viongozi wa makanisa na misitiki wataunda kamati ambao itashughulikia maswala ya usalama.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya serikali ya Marekani kuapa kuisaidia nchi ya Kenya katika kukabiliana na kupambana na ugaidi hususan katika kudhibiti mipaka ya Kenya.

Maisha
Balozi wa Marekani humu nchini Robert Godec alisema mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la kigaidi ya Al Shabaab yatahujumu maisha ya wakenya.

“Tunawapa pole wale wote waliopoteza jamaa zao katika shambulizi la Kanisa. Serikali ya Marekani inashtumu shambulizi hilo. Serikali ya Marekani itawaunga mkono jeshi la Kenya (KDF) ipambane na misimamo mikali wanaotekeleza mashambulizi wanafaa kukamatwa na kushtakiwa” akasema.
Naye Gavana wa Mombasa Hassan Joho akawarai wakazi wa eneo hilo kusimama pamoja na kutotikishwa na shambulizi hilo huku akiapa kwamba lililofanyika halitafanyika tena.

“Hakuna mtu mwenye ruhusa yakuchukua maisha ya mwenzake hususan mtoto mdogo ambaye hana hatia alienda kanisani kuomba tu” akasema.

Akiongeza,” Tunataka waliotekeleza shambulizi hilo wachukuliwe hatua hatutaki watu kupiga domo tu, uchunguzi w akina ufanywe na haki itendeke.”

Akisisitiza kwamba, pigana na nafsi yako! acha uhalifu, acha ulevi, swali, fanya ibada hiyo ndiyo Jihad. Lakini hii kuleta watoto wadogowadogo kuwafundisha uhalifu kuwatia moto waende wapigane na wengine ati jihad? hakuna Jihad sasa, hakuna, Jihad iliisha,  Jihad iliyobaki ni Jihad yako na Mungu wako wewe kama binadamu”. 

Walikuwa wakiongea kwenye halfa la kifua kikuu kaunti ya Mombasa.

0 Responses to “SERIKALI YATOA AMRI YA PIGA "RISASI HADI UUE"”

Post a Comment

More to Read