Monday, March 3, 2014

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUZIDI KUISAIDIA JAMII


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capteni Mstaafu Asseri Msangi Akihutubia Mamia Ya Wakazi wa Mji wa Njombe na Mikoa Jirani Walioshiriki Katika Maadhimisho ya Daraja Day.

 Mkurugenzi wa Shirika la Daraja Mikoa Ya Njombe na Iringa Bwana Saimon Mkina  Akizungumza Mara Baada ya Hotuba Ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

 Mjumbe wa Bodi wa Shirika la Daraja Bi.Josephine Sebastian Lemoyan Akizungumzia Jinsi ya Gazeti la Daraja Letu Linavyofanya Kazi Kubwa Katika Mikoa Ya Njombe na Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Amevitaka Vyombo Vya Habari Mkoani Hapa Kufanya Kazi Kubwa ya Kuendelea Kuibua na Kuandika Mambo Mbalimbali Yaliyojificha Ili Kuisaidia Jamii Kuondoka na Matatizo Yasiyo Ya Lazima.

Capteni Mstaafu Asseri Msangi Ameyasema  Hayo Alipo Kuwa Mgeni Rasmi Katika Maadhimiosho ya Miaka Minne Tangu Kuanzishwa Kwa Kampuni Ya Daraja Letu Katika Mikoa ya Njombe na Iringa.

Capteni Msangi Amesema Kuwa Kutokana na Kuwepo Kwa Changamoto Nyingi Zilizopo Katika Jamii na Kisha Kushindwa Kuifikia Serikali Kwa Wakati Ni Vyema Gazeti la
Daraja Letu Likafanya Kazi Ya Ziada Katika Kuhakikisha Serikali Inayapata Matatizo na Changamoto Hizo Ili Ziweze Kupatiwa Ufumbuzi.

Pamoja na Mambo Mengine Msangi Amelitaka Gazeti Hilo Kuendelea Kuwaandika Viongozi Wabadhilifu,Wanaoshindwa Kutekeleza Majukumu Yao Kwani Kwani Kufanya Hivyo Kutawafanya Kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma.

Sanjari na Hilo Lakini Pia Amesema Mkoa wa Njombe Umekuwa Ukikabiliwa na Changamoto Mbalimbali Ambazo Bila Vyombo Vya Habari Haziwezi Kutatuliwa Huku Akiwataka Wanahabari Kufanya Kazi Zao Kwa Weledi na Kwa Kuzingatia Maadili Ya Uandishi wa Habari Ili Kuepusha Mgongano Baina Ya Viongozi Husika na Wananchi Wanao Waongoza.

Josephine Sebastian Lemoyan ni Mjumbe wa Bodi Ya Kampuni ya Daraja Letu Ambaye Amesema Daraja Letu ni Shirika Linalojishughulisha na Mambo Mbalimbali Ikiwemo Kuibua Miradi Ya Kimaendeleo Katika Jamii Pamoja na Kuitekeleza.

Aidha Bi.Lemoyan Amesema Kuwa Daraja Kupitia Gazeti Lake Limekuwa Likifanya Kazi Kubwa Ambapo Hadi Sasa Limekuwa Likifanya Tafiti Ndogondogo Zinazoendana na Wakati,Kuibua Mambo Yaliyojificha Zikiwemo Changamoto za Sekta ya Elimu,Afya,Miundombinu Pamoja na Huduma za Maji Ambazo Baadhi Zimeweza Kupatiwa Ufumbuzi.

0 Responses to “MKUU WA MKOA WA NJOMBE AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUZIDI KUISAIDIA JAMII”

Post a Comment

More to Read