Monday, March 3, 2014

ATOA MKE WAKE KULIPIA DENI LA SH 17,000




 Kakamega, Raia wa Kenya aliyefahamika kwa jina la Francis Kevogo, amelazimika kumtoa mkewe mwenye umri wa mika 43 ili kufidia deni la sh 900 za Kenya (sh17,100) analodaiwa na kijana wa miaka 22,  Patrick Andambwa.

Taarifa za majirani zinasema kuwa, mwanaume huyo alilazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kushindwa kumlipa Andambwa fedha hizo, walizokubaliana baada ya kumfyatulia matofali.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kevogo aliamua kumlipa Andambwa kwa kumpatia mkewe kama fidia, na kwamba kija huyo alimkubali mwanamke huyo kama fidia ya deni lake.

Habari hizo ziliwashtua wakati wa kijiji cha lwanda kilichopo jirani na daraja la moi katika mpaka  na mji wa Uasin Gishu na kakamega.

Taarifa zaidi zinadaiwa kuwa, mke huyo ambaye alitambulika kwa jina moja la joyce, alikubali kwenda kwa kijana huyo ingawa alikuwa amemzidi umri mara mbili.

“Mume wangu ana tabia mbaya, anakopa watu, kasha anawasingizia kwamba wana uhusiano na mimi na anakataa kuwalipa . hii siyo mara yake ya kwanza” alisema mama huyo.

Joyce aliwaambia waandishi wa habari kwamba, alichukua uamuzi wa kuondoka, na kijana huyo ili kuepuka matatizo na manyanyaso kutoka kutoka kwa mume wake huyo.

0 Responses to “ATOA MKE WAKE KULIPIA DENI LA SH 17,000”

Post a Comment

More to Read