Monday, March 3, 2014
MFUMO WA UPIGAJI KURA KUUAMULIWA NA WAJUMBE WA BUNGE
Do you like this story?
Na mwandishi wetu
Dodoma. Kamati ya watu 20
ya kumshahuri mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalum la katiba, imesema suala la
kupiga kura za siri au za wazi ili kuamua kuhusu vifungu rasimu vya katiba
litaamuliwa na wajumbe.
Ufafanuzi huo ulitolewa
wikiendi iliyopita na mwenyekiti wa wa kamati hiyo, profesa Costa Mahalu baada
ya kuibuka kwa mjadala mkali katika semina ya wajumbe hao iliyojadili rasimu ya
kanuni za bunge hilo iliyofanyika jumatano na alhamis iliyopita, ambapo wengi
wao walipendekeza upigaji kura kuwa wa wazi.
Hata hivyo wazo hili
lilipingwa na baadhi ya wajumbe kutoka vyama vya upinzani na makundi
mbalimbali, wakiwemo wawili hao kutoka chama cha mapinduzi (CCM) ambao ni
Mbunge wa Viti maalum ,Esther Bulaya na
mbunge wa urambo magharibi, profesa Juma Kapuya.
Akitoa ufafanuzi wa
mapendekezo ya wajumbe hao, profesa mahalu alisema “jambo hili limetusumbua
kwenye kamati. Wakati tukifanya uchambuzi tuliona aina zote mbili za upigaji wa
kura ni mchakato wa kidemokrasia na zote hazizuii haki ya kupiga kura”.
Alisema wote waliochangia
suala hili walikuwa na hoja za msingi na kuongeza kutokana na wajumbe kuw na
mawazo tofauti, kamati ilipendekeza suala hilo liamuliwe na wajumbe wenyewe”
Profesa Mahalu alisema
kitachoamuliwa na wajumbe hao ndicho kitakachochukuliwa na kuingizwa katika
kanuni hizo. Kuhusu marekebisho mengine, profesa mahalu alisema mijadala
itakayokuwa ikifanyika katika kamati za bunge maalum, waandishi wa habari
wataruhusiwa kuingia.
“Mijadala ya kamati
itakuwa wzi kupitia vyombo vya habari isipokuwa wataalamu wanaweza kualikwa
kwaajili ya kutoa ushauri “alisema.
Alizungumzia kuhusu
utaratibu DK Rehema Nchimbi wa kumwondoa
mwenyekiti na makamu wa Bunge profesa Mahalu alisema mwenye lengo hili ni lazima
apate saini za wajumbe wasiopungua nusu ya wabunge wote wa bunge hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MFUMO WA UPIGAJI KURA KUUAMULIWA NA WAJUMBE WA BUNGE”
Post a Comment