Monday, March 3, 2014
WAJUMBE TISA HAWAJARIPOTI BUNGENI
Do you like this story?
BUNGE LA KATIBA DODOMA |
Wakati
wajumbe tisa kati ya 629 wan Bunge maalum la katiba, hawajaonekana bungeni
tangu lilipoanza shughuli zake February 18 mwaka huu, Ikulu imesema kuwa Rais
Jakaya Kikwete hawezi kuwachukulia hatua na badala yake wenye uwezo huo makundi
wanayotoka.
Mkurugenzi
Msaidizi wa bunge (Habari), Deogratis Egidio alisema juzi kuwa, wajumbe watatu
miongoni mwa wajumbe hao tisa, wanatoka kundi la baraza la wawakilishi, wane wa
jamhuri na wawili ni wateule wa Rais.
“Ili
mjumbe wa bunge hili atambulike kuwa amehudhuria vikao ,lazima afanyiwe
usajili, kufunguliwa jalada maalumu na badaye kurejeshewa gharama za nauli na
malipo ya posho zake. “ Baraza la wawakilishi lina wajumbe 77 na kati yao,
watatu bado hawajaripoti. Kati ya wajumbe wane wa kundi la bunge la jamhuri
ambao hawajaripoti, wawili ni wagonjwa mmoja ana udhuru wa kikazi na mwingine hatuna taarifa naye”
alisema Egidio.
Wajumbe
wa bunge la jamhuri amabo hawajaonekana tangu kuanza kwa bunge hili ni pamoja
na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya ambaye Egidio alisema wana taarifa naye na
mwingine ni mbunge wa singida Mjini, Mohamed Dewji ambaye bunge halina taarifa zake.
Alisema
wabunge 201 wa kuteuliwa waliofika katika bunge hilo ni 199, na ambao
hawajafika ni wawili; Omary Hussein na zainab Bakari Dihenga’
Ikulu yazungumzia wabunge ‘watoro’
Katibu
Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni sefue alisema ingawa Ikulu haina taarifa rasmi
kutoka ofisi za bunge maalum kuhusu mahudhurio hayo, lakini siyo jukumu la Rais
kuwalazimisha wahusika wahudhurie Bunge.
Alisema
kwa sababu wajumbe hao waliteuliwa na Rais kutokana na kupendekezwa na makundi
yao, ni vyema makundi hayo yawabane watu hao kuingia bungeni .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAJUMBE TISA HAWAJARIPOTI BUNGENI”
Post a Comment