Wednesday, March 26, 2014
MTOTO ALIYEJERUHIWA KATIKA SHAMBULIO KANISANI AFIKISHWA NAIROBI KWA MATIBABU.
Do you like this story?
Mtoto Satrin Osinya wakati akipatiwa matibabu
mjini Mombasa baada ya kupigwa risasi.
|
Mtoto Satrin akiwa amebebwa na baba yake mzazi Benson Osinya ndani ya ndege kuelekea jijini Nairobi kwa matibabu. |
Kaka wa Satrin Osinya, Moses Gift akiwa amembeba mdogo wake baada ya kunusurika kifo. |
MTOTO Satrin Osinya aliyejeruhiwa na risasi
iliyomuua mama yake katika shambulio la kigaidi lililofanywa kwenye kanisa la
Joy of Jesus huko Likoni, Mombasa nchini Kenya Jumapili iliyopita, jana
amefikishwa jijini Nairobi kwa matibabu.
Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu
anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa katika Hospitali Kuu ya Kitaifa ya
Kenyatta ili kuondoa risasi iliyoingia kwenye ubongo wake baada ya kumuua mama
yake.
Madaktari wanasema kuwa ubongo wa mtoto huyo umefura na kwamba risasi iko upande wa kulia wa ubongo wenyewe. Upasuaji unatarajiwa kufanywa baada ya wiki mbili ambao utagharamiwa na serikali
Madaktari wanasema kuwa ubongo wa mtoto huyo umefura na kwamba risasi iko upande wa kulia wa ubongo wenyewe. Upasuaji unatarajiwa kufanywa baada ya wiki mbili ambao utagharamiwa na serikali
Mama
mzazi wa Satrin aliyekuwa akijaribu kumkinga mwanaye kutoka kwa magaidi
waliovamia kanisa la Joy of Jesus siku ya Jumapili, alifariki kanisani humo
baada ya kupigwa risasi. Inadaiwa risasi aliyomuingia kichwani Satrin ni risasi
iliyomuua mama yake kupitia kifuani na kuishia katika ubongo wa mtoto huyo.
Mamake Satrin, alikuwa miongoni mwa watu sita waliouawa katika shambulizi hilo, baada ya washukiwa watatu wa ugaidi kulivamia kanisa hilo katika mtaa wa Likoni na kuanza kuwafyatulia waumini risasi kiholela.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTOTO ALIYEJERUHIWA KATIKA SHAMBULIO KANISANI AFIKISHWA NAIROBI KWA MATIBABU.”
Post a Comment