Wednesday, March 26, 2014
HII NDIO TIMU YA WATOTO WA MTAANI TANZANIA ILIVYOONDOKA LEO KWENDA BRAZIL KUCHEZA KOMBE LA DUNIA.
Do you like this story?
TIMU
ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza imeondoka leo (Machi
26 mwaka huu) kwenda Brazil kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto
wa Mitaani.
John Kadutu ambaye ni
mjumbe wa Bodi ya kituo hicho, na pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha klabu za Mkoa wa Mwanza ndiye
kiongozi wa msafara wa timu hiyo ya Tanzania. Michuano hiyo ya siku 10 inayoshirikisha
watoto wa mitaa (wavulana na wasichana) inaanza keshokutwa (Machi 28 mwaka
huu). Nchi 19 zinashiriki michuano hiyo itakayofanyika katika Jiji la Rio de
Janeiro.
Mbali ya Tanzania, nchi nyingine zinazoshiriki michuano hiyo
kwa upande wa wavulana ni Argentina, Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani,
Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El
Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe. Mwaka
2010 mashindano hayo yalifanyika Durban, Afrika Kusini ambapo pia Tanzania
ilishiriki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HII NDIO TIMU YA WATOTO WA MTAANI TANZANIA ILIVYOONDOKA LEO KWENDA BRAZIL KUCHEZA KOMBE LA DUNIA.”
Post a Comment