Wednesday, March 26, 2014

RAIS AVUNJA TUME YA KATIBA.




Rais Jakaya Kikwete amevunja rasmi tume ya mabadiliko ya katiba  badala ya tume  hiyo kumaliza kazi iliyopewa na kukabidhi  rasimu ya katiba  kwa bunge maalumu.

Kwa mujibu taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano  ikulu Rais  aliunda tume hiyo kwa muibu wa kifungu cha 5 na cha 6  cha sheria  ya mabadiliko ya katiba  sura ya 83  kwa tangazo la serikali na. 110 la mwaka 2012.

Makukumu ya tume hiyo yalikuwa ni ya pamoja na kukusanya maoni kwa wananchi  na kuandaa rasimu ya katiba  ya jamhuri ya muungano wa Tanzania  kazi ambayo imefanywa na tayari  imeshwawalishwa kwenye bunge  maalumu la katiba.

Tarifa hiyo ilisema kwa mujibu  wa kifungu cha 31 cha sheria ya mabadiliko ya katiba sura ya 3 Rais alipewa mamlaka ya kuvunja tume ya mabadiliko ya katiba baada ya rasimu ya katiba  kuwasilishwa bungeni.

Na kwamba mchi 18 mwaka huu mwenyekiti  wat ume hiyo jaji joseph warioba  aliwasilisha rasimu ya katiba kwenye bunge maalum. Hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 31  cha sheria ya mabadiliko ya katiba rais alivunja rasmi tume hiyo machi 19 mwaka huu kwa tangazo   la serikali  namba 81 la machi 21, 2014.

Hivyo kwa tangazo  hilo shughuli zote za tume  ya mabadiliko  ya katiba zimemalizika  rasmi tarehe 19 machi 2014.

0 Responses to “RAIS AVUNJA TUME YA KATIBA.”

Post a Comment

More to Read