Wednesday, March 26, 2014

WARIOBA AFUNGUKA.




Wakati Ikulu  ikitangaza kwamba Rais kikwete  amevunja tume ya mabadiliko  ya katiba, tume  hiyo imetoa ufafanuzi wa baadhi ya maneno  ya rasimu ya katiba.

Taarifa ya ikulu iliyotolewa jana ilieleza kuwa tume ya jaji joseph warioba ilivunjwa tangu machi 19  ikiwa ni siku moja baada  ya kuwasilisha rasimu  ya katiba bungeni  mjini Dodoma.

Wakati taarifa ya tume ya warioba  ilitolewa jana jioni  kurugenzi ya mawasiliano ya Rais , Ikulu ili kuwa imetosa taarifa  ya kuvunja tume hiyo mapema jana ikileza kuwa shughuli za tume hiyo zilikoma tangu jumatano  iliyopita.

Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha sheria ya mabadiliko ya katiba Rais wa jamhuri ya muungano  alivunja rasmi tume ya mabadiliko ya katiba tarehe 19  machi 2014 kwa tangazo la serikali na.81 la tarehe 21 machi  2014 ilisema taarifa hiyo ya Ikulu.

Hata hivyo jaji warioba amesema jana kuwa hadi wanakutana  juzi kwenye kikao cha mwisho tathmini walikuwa hawajapokea barua ya kuvunjwa kwa tume yake.

Barua ya Ikulu tumeipokea leo. Tulukuwa hatuna  taarifa kwamba tume yetu imevunjwa  hadi tulipopokea barua  leo (Jana) tulifanya kikao chetu cha mwisho cha tathimini jana (juzi) alisema warioba alipozungumza na mwananchi jana jioni.

Warioba pia alithibitisha kwamba tarifa ya ufafanuzi (imechapishwa ukurasa 37) ni ya tume ya mabadiliko ya katiba.

Taarifa hiyo ya tume ya warioba imetaja baadhi ya sababu za kupendekezwa kwa muundo wa serikali tatu kuwa ni pamoja na serikali ya muugano  kutokuwa tena na nguvu  upande wa Zanzibar na Rais  kupokwa  baadhi ya madaraka aliyopewa kikatiba.

0 Responses to “WARIOBA AFUNGUKA.”

Post a Comment

More to Read