Wednesday, March 26, 2014

KENYATTA ATAJA CHANGAMOTO EAC.




Rais uhuru Kenyatta wa Kenya amesema moja ya changamoto  zinazoikbaili jumuiya  ya Afrika Mashariki (EAC) ni uchumi duni miongoni mwa nchi wananchama.

Akihutubia bunge la Eela  jijini Arusha jana Rais Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa wakuu wa EAC  amesema ili kujikwamua nchi za kiafrika lazima zijiendeleze  kwenye mapinduzi  ya viwanda na kujijengea uwezo  wa kuongeza thamani bidaa zake badala ya  kusafirisha nje malighafi.

Kuongeza thamni  bidhaa zetu kabla ya kuzisafirisha licha ya kukuza uchumi w etu lakini pia  kutaongeza fursa za ajira kwa vijana tofauti na sasa ambapo  ajira hizo hupelekwa nje amesema Kenyatta.

Amesema jambo la msingi katika mapinduzi ya kiuchumi ni umoja  na ushirikiano  miongoni mwa wananchi wa EAC na Afrika  kwa ujumla na kutaka viongozi waliokabidhiwa dhamana kuongoza kwa vitendo  badala ya maneno.

Changamoto zingine zinazopaswa  kushughulikiwa  kwa ajili ya ustawi  wa umma wa EAC  kwa mujibu wa Rais Kenyatta  ni vikwazo  vya kibiashara  na usafiri  miongoni  mwa nchi wanachama.

Amesema nchi za EAC hazina budi kukabiliana na kupunguza gharama za biashara kulingana na mikataba ya ushuru wa forodha.

0 Responses to “KENYATTA ATAJA CHANGAMOTO EAC.”

Post a Comment

More to Read