Wednesday, March 26, 2014

RC MARA AFARIKI DUNIA GHAFLA.




Mkuu wa mkoa wa mara john tuppa afariki dunia baada  ya kuanguka ghafla  kutoka kwenye kiti alichoketi wakati akishiriki kikao cha kamati ya ulinzi na usalama  wilayani tarime.

Taarifa kutoka ndani ya kikao zilidai  kuwa kabla  ya kufikwa na mauti  tuppa alisalimiana na wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuanza kikao.

Baada ya kuanguka alipelekwa  katika hospitali ya wilaya ya tarime ambako alifariki dunia wakati  akipewa matibabu.

 Kikao hicho kilikuwa maandalizi  ya kukabidhi vyeti  kwa vijana waliomaliza mafunzo ya mgambo kijiji  cha nyamwaga  wilayani tarime mafunzi hayo yameandaliwa  na kikundi cha uliinzi cha  nyabigenda security  cooperative ltd.

Akitangaza  kifo hicho katibu tawala mkoa wa mara  bendicto ole kuyani  amesema tuppa alionekana mwenye afya njema  jana asubuhi kabla  ya kuelekea tarime kikazi.

Kuyani amesema tuppa hakuwa na historia ya kusumbuliwa na ugonjwa wowote ingawa taarifa  zisizo  rasmi zilidai kuwa chanzo  cha kifo ni shinikizo la damu.

 Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya tarime, DK nega nyakabogo alithibitisha  kifo hicho . “tulimpokea  akiwa kwenye

0 Responses to “RC MARA AFARIKI DUNIA GHAFLA.”

Post a Comment

More to Read