Wednesday, March 26, 2014

WANAWAKE WAHUSISHWA NA JINSIA ZA KIUME.




Mjumbe wa bunge la katiba faida bakari amelalamika baadhi ya wajumbe  wanawake  kuandikwa  ni wanaume katika orodha  ya kamati za bunge  iliyotangazwa  mjini Dodoma.

Akizungumza bungeni faida alitaja baadhi ya majina yaliyoandikwa  kuwa ni wanaume ni muhonga ruhanywa na asma  ali na kimsingi hili limemkera.

“majina  haya  yaangaliwe upya wanawake wameandikwa ‘me’ (wanaume) inawezekana na wanaume  wameandikwa ‘ke’ (wanawake) alisema.

Akijibu hoja hiyo mwenyekiti wa bunge Samuel sitta alitaka sekretarieti  kuangalia na kusahihisha jambo hilo.

0 Responses to “WANAWAKE WAHUSISHWA NA JINSIA ZA KIUME.”

Post a Comment

More to Read