Wednesday, March 26, 2014

BWANA YESU ASIFIWE YAMKERA KINGUNGE.




Mjumbe wa bunge la katiba kingunge  ngombale mwiru amesema salamu za wanasiasa   zinamkera kwa kuwa  wanafanya wasilolijua.

Salamu iliyomkera  kingunge ni kwa baadhi ya watu kusema “Bwana yesu asifiwe”  au “Tumsifu yesu kristo”  ambazo alisema ni salamu za kitumwa lakini akasifia  salamu ya Assalaam Aleykum.

Kingunge ambaye anajulikana kama muumini  mkubwa wa siasa ya ujamaa alitoa kauli hiyo katika semina  ya waandishi wa habari  kuhusu wajibu wao katika kuripoti bunge la katiba iliyoandaliwa  na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Mkongwe huyo ni mmoja wa watu ambao wasio na imani ya dini na mara zote  amejipambanua kuwa  haamini hilo na hata katika viapo vyake hatumii  kitabu chochote cha dini.

“Salamu ya ‘bwana Asifiwe’ Au Tumsifu yesu kristo ni matokeo ya utumwa  ambayo mimi nimekuwa nikikerwa  hasa kwa wanasiasa ambao wanapenda  kuitumia alisema kingunge.

“Sisi tangu zamani tunajua kuwa Assalam Aleykum ni amko la amani ambalo lilikuwepo kabla ya mtume  kuliko hizo nyingine ambazo hata ndani ya CCM wanafanya hivyo wakidhani ni sahih”

Salmu hiyo hutumiwa na waumini wa kikristo lakini pia katika mikutano mbalimbali ya kisiasa.

0 Responses to “BWANA YESU ASIFIWE YAMKERA KINGUNGE.”

Post a Comment

More to Read