Wednesday, March 26, 2014
TUNAMWONEA BURE JAJI WARIOBA.
Do you like this story?
Nchi hii kwa kweli ina visa sijawahi kuviona
mahali kwingine katika dunia hii. Ni nchi ya ajabu na sijui ilikuwaje nikaishi
humu.
Kuna mambo mengi yanayotokea na kunilazimisha
baadhi ya nyakati kulaani kwa nini nimekuwa Mtanzania, yaani inachosha sana.
Hivi sasa kuna hizi harakati za kutafuta
Katiba mpya hapa nchini. Iliundwa tume maalumu ya kutusaidia kupata katiba
hiyo.
Watu kutoka makundi mbalimbali wakateuliwa,
wakiwamo wanasiasa kutoka chama tawala cha CCM na hata vyama vya upinzani.
Makundi mengine nayo yakashirikishwa ipasavyo. Baada ya kumaliza kazi yake,
tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mzee Joseph Warioba ilikabidhi rasimu zake kwa
Serikali na kwa wananchi kwa jumla.
Sasa kioja kimeanza kutoka kwa wanasiasa hasa
wale wa CCM ambao kila siku wanamsimanga mzee wa watu bila sababu yoyote.
Kila siku Mzee Warioba yuko midomoni mwao
wakimlalamikia kwa hili ama lile.
Utafikiri kuwa maoni yaliyomo kwenye rasimu
yaliandaliwa na Mzee Warioba chumbani. Tume ilikuwa na wajumbe kibao tena
wengine ni kutoka CCM, lakini mzigo wote ni Warioba, kila mtu Warioba kama vile
yeye ndiye aliyetengeneza rasimu hiyo.
Kama CCM hawakubali mawazo ya wananchi waliyotoa
kwa wajumbe wa tume, basi wasimwonee Warioba pekee, wawe pia wanawataja wajumbe
wengine tunaojua kuwa nao ni CCM wa damu.
Huyu mzee kaitumikia nchi hii kwa uadilifu
mkubwa, jamani aachwe apumzike kwa amani. Kwa nini tumchoshe?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TUNAMWONEA BURE JAJI WARIOBA.”
Post a Comment