Wednesday, November 11, 2015
CCM LUDEWA YAMPITISHA NGALAWA KUWANIA UBUNGE
Do you like this story?
SIKU ya jana haikuwa nzuri kwa baadhi ya ndugu, jamaa na
marafiki wa familia ya marehemu Deo Filikunjombe baada ya mdogo wake Phillip
Filikunjombe kushika nafasi ya pili katika kura za maoni ya ubunge wa jimbo la
Ludewa zilizofanyika jana, mjini Ludewa.
Uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo uliahirishwa baada ya
aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo, Deo Filikunjombe kufariki dunia katika ajali
ya helikopta iliyotokea Oktoba 15, siku 10 kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu.
Phillip Filikunjombe aliyekuwa anategemewa na wengi kushinda
kura za maoni za jimbo hilo ili aingie moja kwa moja katika kinyang’anyiro cha
ubunge wa jimbo hilo lililoongozwa na kaka yake Deo katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita, amepata kura 501 akizidiwa na Deo Ngalawa aliyepata kura 537.
Filikunjombe aliangushwa na mgombea mwenzake huyo katika
kinyang’anyiro kilichoshikilisha wagombea saba, baada ya wengine watatu kujitoa
kwa ombi la kumuunga mkono Filikunjombe.
Waliojitoa katika kinyang’anyiro hicho
kilichomshilikisha msanii wa vichekesho na muimbaji wa nyimbo za injili,
Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la ‘Masanja Mkandamizaji’ aliyeambulia kura
19 ni pamoja Johnson Mgimba na Simon Ngatunga.
Wengine walioshiriki kura hizo za maoni na kura zao kwenye
mabano ni James Mgaya (72), Dk Evaristo Mtitu (21) na Zephania Chaula (21) na
Mpangala Mpangala (3).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CCM LUDEWA YAMPITISHA NGALAWA KUWANIA UBUNGE”
Post a Comment