Wednesday, November 11, 2015
JB ALISHWA SUMU!
Do you like this story?
Habari mbaya iliyolifikia imeeleza kwamba,
staa wa sinema za Kibongo, Jacob Stephen ‘JB’ amenusurika kifo baada ya kudaiwa
kulishwa sumu na kujikuta katika hali mbaya kiafya kabla ya kukimbizwa
hospitalini.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa JB, masaibu hayo yalimkuta wikiendi iliyopita akiwa katika mishemishe zake kwenye viunga mbalimbali vya Jiji la Dar.
Inadaiwa JB alizidiwa Jumamosi iliyopita
alipoanza kulalamika kukatwa na tumbo, lakini wenzake wakachukulia poa na
kumshauri kwenda kuchukua vipimo hospitali.
“Baada ya vipimo alipewa dozi akarudi
nyumbani lakini asubuhi yake (Jumapili), hali ilizidi kuwa mbaya zaidi ndipo
akakimbizwa Hospitali ya Marie Stopes (Mwenge, Dar).
kuzungumza na baadhi ya wauguzi ambao
walikiri JB kufikishwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya.
“Madaktari waligundua kwamba alikuwa
amelishwa sumu lakini mwenyewe alikuwa haelewi alichopewa kwa sababu alisema
alikuwa amekula vitu mbalimbali tena sehemu tofauti,” alisema mmoja wa wauguzi
hao ambaye aliomba hifadhi ya jina.
Akizungumza na waandishi wa Habari, JB ambaye
kwa muda mrefu alikuwa akizunguka mikoani kwenye kampeni za uchaguzi alisema
kuwa alishangaa kujikuta akishindwa kuendelea na ratiba zake za kazi kufuatia
kusumbuliwa na tumbo lililokuwa likimkata kabla ya kugundulika kuwa alilishwa
chakula chenye sumu.
“Namshukuru Mungu naendelea vizuri lakini
hali ilikuwa mbaya mno, bado sijaweza kutoka ndani naendelea na dozi,” alisema
JB akiomba aendelee kupumzika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JB ALISHWA SUMU!”
Post a Comment