Friday, May 23, 2014

JEURI YA PESA HIYO!, PSG WATAKA KUMSAJILI DAVID LUIZ KWA DAU LA PAUNDI MILIONI 50 NA KUVUNJA REKODI YA DUNIA



Nyota wa Chelsea,  Luiz yuko njia kuelekea PSG kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 50.


NDANI ya saa 48 zajazo, David Luiz anaweza kujiunga na Paris St Germain kwa dau nono la paundi milioni 50.

 Kiwango halisi cha ada ya uhamisho kitatajwa na klabu, lakini uhamisho wa beki huyo wa Chelsea mwenye miaka 27 utavunja rekodi ya dunia kwa uhamisho wa mabeki.

PSG iliweka rekodi ya kuwasajili mabeki wawili Marquinhos na Thiago Silva kwa dau nono zaidi, lakini kama watamnasa Luiz kwa mkwanja huo watavunja rekodi hiyo.

Kama dau hilo litakubaliwa  Stamford Bridge, PSG wataomba ruhusa kwa kocha wa Brazili Luiz Felipe Scolari ili wakamchukua vipimo vya afya wakati huu anapojiandaa na kombe la dunia.

PSG  wanaamini kumsajili Luiz watakuwa wamefanikiwa kusajili beki bora zaidi duniani na usiku wa jana walionekana kuwa tayari kulipa kiwango chochote watakachohitaji Chelsea.
Matajiri hao wa Ufaransa wanataka kuonesha umwamba wao wa kifedha kwa mara nyingine tena majira ya kiangazi.

Vyanzo vya habari mjini Paris vimethibitisha kuwa PSG wanajipanga mapema kuwapiga bao Barcelona na Bayern Munich wenye nia ya kumsajili.

Na inaaminika kuwa kwa dau hilo PSG hawana mpinzani. 
Chelsea watatumia fedha hizo kuimarisha kikosi chao kwa kumchukua nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa.

0 Responses to “JEURI YA PESA HIYO!, PSG WATAKA KUMSAJILI DAVID LUIZ KWA DAU LA PAUNDI MILIONI 50 NA KUVUNJA REKODI YA DUNIA”

Post a Comment

More to Read