Friday, May 23, 2014
TAARIFA KWA UMMA KULAANI KITENDO CHA KUMFICHA MTOTO NASRA (4) CHUMBANI NA KUMFUNGIA NDANI YA KASHA KWA MUDA WA MIAKA MINNE ENEO LA KIWANJA CHA NDEGE, MANISPAA YA MOROGORO
Do you like this story?
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
|
(PRESS RELEASE)
Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto inalaani vikali tukio la ukatili na udhalilishaji dhidi ya
mtoto Nasra (4) mkazi wa mjini Morogoro ambaye alifichwa chumbani ilhali
amefungiwa ndani ya kasha na mama yake mkubwa kwa muda wa miaka nne, baada ya
mtoto huyo kufiwa na mama yake mzazi.
Kitendo hicho ni ukiukwaji wa
haki za mtoto. Wizara inasisitiza kwamba mzazi au mlezi yeyote anayekubali
jukumu la kulea mtoto anaowajibu wa kuhakikisha kuwa anampatia mahitaji yote
muhimu ya kumwezesha mtoto kukua hadi kufikia utimilifu wake. Wizara inakemea
vikali kitendo hicho na vingine vingi vya aina hiyo ambavyo vinaendelea
kufanyika katika familia zetu na jamii kwa ujumla.
Wizara inaziomba mamlaka
zinazohusika na udhibiti wa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kuhakikisha
kuwa watuhumiwa wote wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili haki iweze
kutendeka na kuwa fundisho kwa wanaoendeleza ukatili dhidi ya watoto. Jamii
inahimizwa kubadilika na kuhakikisha kuwa familia ambayo ndio kitovu cha jamii
panakuwa ni mahala salama; na kuwahakikishia watoto haki zao za msingi
ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushiriki na kutobaguliwa.
Wizara inapongeza Uongozi wa
Manispaa ya Morogoro hasa Afisa Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi kupitia Dawati
la Jinsia na Watoto na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege kwa
kufuatilia suala hili kwa karibu. Vile vile, Wizara inapongeza majirani na
vyombo vya habari kwa uzalendo wao mkubwa wa kufichua ukatili aliofanyiwa mtoto
huyu maana taarifa zao zimesaidia kunusuru uhai na maisha ya mtoto Nasra.
Wizara inamwelekeza Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Morogoro awasiliane na Afisa Ustawi wa Jamii
husika kuona uwezekano wa kumkabidhi mtoto Nasra kwenye taasisi zinazohusika na
matunzo ya watoto ili awe kwenye mikono salama, wakati taratibu za kisheria
zikifanyika dhidi ya wanaohusika na ukatili huo.
Anna T. Maembe
KATIBU MKUU
23 Mei, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA KWA UMMA KULAANI KITENDO CHA KUMFICHA MTOTO NASRA (4) CHUMBANI NA KUMFUNGIA NDANI YA KASHA KWA MUDA WA MIAKA MINNE ENEO LA KIWANJA CHA NDEGE, MANISPAA YA MOROGORO”
Post a Comment