Tuesday, May 6, 2014
RAGE `BAI BAI` SIMBA SC, WANACHAMA KAZI KWENU KUPATA MRITHI WA MIKOBA.
Do you like this story?
MWANASHERIA Damas Ndumbaro amepewa jukumu la kuongoza kamati ya
uchaguzi wa Simba sc kwa lengo la kupata warithi wa viongozi wasasa
wanaoongozwa na mwenyekiti, Ismail Aden Rage.
Kamati ya uchaguzi imeanza kazi hiyo
baada ya serikali kukabidhi katiba iliyofanyiwa marekebisho kwa uongozi wa
Simba sc.
Uchaguzi wa Simba ulitakiwa kufanyika
wiki iliyopita, lakini mapungufu katika vipengele kadhaa katika katiba yao
yalikwamisha .
Lakini jana katibu mkuu wa Simba sc,
Ezekiel Kamwaga alitangaza kuwa tayari serikali imemaliza zoezi lake na
kukabidhi katiba.
Kwa misingi hiyo, Kamati ya uchaguzi
haina cha kupoteza zaidi ya kuanzisha rasmi mchakato mzima wa kupata viongozi
wapya wa klabu.
Tangu Rage aingie madarakani miaka
miwili iliyopita kumekuwepo na changamoto nyingi na mivutano isiyoisha.
Si rahisi kujua kama Rage alikuwa mbaya
katika uongozi wake kwasababu inasemekana kuna watu wachache walikuwa
hawampendi ndani ya uongozi na kupandikiza chuki kwa wanachama ili aonekane
hafai.
Majaribio kadhaa ya kutaka kumpindua
Rage yameshuhudiwa bila mafanikio.
Katiba ya Simba imekuwa ikimlinda kwa
wakati wote, hivyo wale wanaojaribu kumpindua kugonga mwamba.
Unakumbuka sakata la aliyekuwa kaimu
mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang`are `Mzee Kinessi` na baadhi ya wajumbe wa
kamati ya utendaji.
Kinessi alitangaza kumsimamisha
mwenyekiti Rage, lakini mwanaume huyo aliyekuwepo nje ya nchi alirudi na kuita
kikao chao kama kikao cha harusi na yeye atabaki kuwa mwenyekiti.
Hata TFF walitangaza kumtambua na
akaendelea na majukumu yake klabuni.
Pia wanachama wa baadhi ya matawi
walishakutana mara kadhaa kutaka kumpindua Rage, lakini waliishia kuzodolewa na
mkuu wao huyo.
Rage aliweza kuyafanya hayo kwa misingi
ya katiba ya Simba waliyoiandika wanachama wenyewe.
Wakati Rage anaingia madarakani,
alikuja na mipango mizuri ili kuiweka Simba klabu ya kisasa.
Aliahidi kujenga uwanja mzuri wa klabu,
lakini ndoto zake ziliyeyuka baada ya kutokea migogoro.
Inasemekana kuna watu walimsaliti Rage
na kufanya kazi ya kueneza sumu kwa wanachama. Ni ngumu kubaini hayo kwasababu
mambo mengine yapo chini ya kapeti.
Inawezekana Rage ana mapungufu yake
kama ilivyo kwa binadamu yeyote, lakini namna ya kujua mapungufu haya lazima
uwe na hoja iliyojengwa kwa umakini mkubwa.
Rage kaifanyia mengi klabu yake, lakini
kwasababu watu wengi wanaamini hafai, basi yanaokena mabaya zaidi kuliko
mazuri.
Hakuna haja ya kuumiza kuzungumza juu
ya Rage ambaye tayari ameshatangaza kutogombea tena katika uchaguzi ujao.
Wanachama wa Simba umefika muda wa
kumtoa madarakani Rage ambaye wengi wenu mnaona hafai kwa mujibu wa katiba.
Klabu zinazoendeshwa na wanachama kama
ilivyo kwa Simba na Yanga, wa mwaka au mkutano mkuu wa uchaguzi ndio kila kitu.
Sasa Rage anaondoka, kazi kubwa ni
kumpata mrithi wake wa kuendeleza mazuri yake na kufuta mabaya yake.
Kama kwa muda mrefu mlikuwa mnataka
mpiganaji Rage aondoke Simba, umefika wakati wa yeye kukaa pembeni.
Kumbukeni soka limebadilika nchini
Tanzania. Kwa mipango mibovu, Simba imemaliza nafasi ya nne msimu uliopita.
Msimu wa mwaka juzi mlimaliza nafasi ya
tatu. Kwa misimu miwili mnakosa michuano ya kimataifa.
Najua mnaikumbuka Simba yenu ya 2003 na
ile ya akina Okwi misimu miwili iliyopita.
Simba ilikuwa hatari sana, lakini siku
za karibuni imekuwa na matokeo mabaya na sasa kuanza kuonekana timu ya kawaida.
Zamani timu kukutana na Simba ilikuwa
shughuli pevu, lakini msimu uliopita watu walikuwa wanajipigia kirahisi.
Ni kweli Simba mpo kwenye mpito
kwasasa. Lakini wakati wa mabadiliko umeshawadia.
Kwa muda mrefu wachezaji wa Simba
wamekuwa wakilalamika chini kwa chini kuwa uongozi wa Rage umeshindwa kuboresha
mishahara yao.
Pia ucheleweshaji wa mishahara na posho
imekuwa tatizo. Hata siku wakienda Zanzibar kujianda na mechi ya Yanga,
wachezaji kwa saa kadhaa waligoma kuingia kwene boti kwa kushinikiza kulipwa pesa
zao.
Zacharia Hans Poppe aliokoa jahazi na
tuliona mpira wenu mkubwa uwanja wa Taifa na Yanga ambapo wanajangwani
walihangaika kuchomo o bao na kulazimisha sare ya 1-1.
Pia kumekuwepo na mabadiliko ya
mfufulizo katika benchi la ufundi, hivyo kuleta athari kubwa.
Simba imekuwa ikienda mbele na kocha
huyu, lakini ghafla analetwa mwingine na falsaya mpya na kuanza upya.
Bahati nzuri kocha wa sasa, Dvrako
Logarusic ameaminiwa na ataandeleza pale alipofikia mwaka huu na tayari
ameshakabidhi ripoti yake na mapendekezo ya usajili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAGE `BAI BAI` SIMBA SC, WANACHAMA KAZI KWENU KUPATA MRITHI WA MIKOBA.”
Post a Comment