Friday, March 28, 2014
SIMBA 4 NA TWIGA 1 WALIULIWA DENMARK.
Do you like this story?
Hifadhi moja ya wanyamapori
iliyowagadhabisha watu kwa kumuua Twiga nchini Denmark mwezi jana, imewaua
Simba wanne ili kutoa nafasi kwa Simba mmoja mgeni anayetarajiwa kuletwa katika
mbuga hiyo hivi karibuni
Wasimamizi wa hifadhi hiyo mjini
Copenhagen, waliwaua Simba wawili wadogo na wawili wakubwa walio wazaa wadogo
hao baada ya kukosa nafasi ya kuwahifadhi.
Hifadhi hiyo ilisema kuwa Simba hao
wakubwa waliokuwa na miaka 16 na 14, walikuwa wamefikisha umri wa kupekwa
mbugani.
Mwezi jana hifadhi hiyo ilimuua
Twiga mkubwa mwenye afya tele kwa sababu alionekana kuwa na mahitaji mengi
kuliko uwezo wa hifadhi hiyo.
Taarifa kutoka katika hifadhi hiyo
ilisema kuwa kwa sababu Simba walikuwa wakubwa walihitaji kuuawa huku wadogo
wakiuawa kwani hawana uwezo wa kujilisha bila ya wazazi wa
Twiga aliyeuawa alikuwa kitoweo kwa
Simba wengine katika hifadhi hiyo
Kulingana na wasimamizi, Simba huyo
mgeni angeuawa na Simbawakubwa kwa sababu ndio kawaida ya wanyama hao kuua wale
ambao hawajawaza.
Walisema kuwa walikuwa wametoa ombi
kwa hifadhi zengine kumchukua Simba huyo mchanga lakini hakuna yeyote
aliyekubali kufanya hivyo.
Simba huyo mgeni anapaswa kuwasili
katika hifadhi hiyo katika siku chache zijazo na atakaribishwa na simba wawili
wa kike waliozaliwa mwaka 2012 na ambao wako tayari kuzaa.
Mwezi jana mkuu wa hifadhi hiyo,
alitishiwa maisha yake baada ya kumuua Twiga huyo ambaye baadaye alifanyiwa
upasuaji mbele ya umati wa watu.
Watu duniani kote hasa wapenzi wa
wanyama wa porini, walighadhabishwa mno na hatua ya kuuawa kwa Simba hao na
Twiga.
Licha ya kilio cha wengi, mbuga hiyo
ilisema kuwa haiko tayari kubadilisha taratibu zake za kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMBA 4 NA TWIGA 1 WALIULIWA DENMARK.”
Post a Comment