Sunday, March 30, 2014
SPIKA ANNA MAKINDA ATOA DARASA KWA WANAWAKE KUCHANGIA HOJA ZA NGUVU KWENYE BUNGE LA KATIBA.
Do you like this story?
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Anne Makinda ametoa changamoto kwa
wajumbe wenzake wanawake walio kwenye Bunge hilo, kujenga hoja zenye nguvu
zinazohusu masuala yanayohusu wanawake na kuzitetea kwa sauti
moja ili ziweze kupita katika Rasimu ya Katiba.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe. Anne ambaye pia ni Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akitoa mchango
wake kwa wajumbe wa semina ya kujenga agenda
muhimu kwa masuala ya kijinsia iliyoandaliwa na Umoja wa
Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (TWPG)
kwa wajumbe wanawake wa Bunge hilo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa.
“ Ninawaomba tuwe na hoja zenye nguvu wakati wakuchangia
mjdala wa Rasimu ya Katiba . Tukisimama kwa hoja za nguvu na kutetea
vifungu vinavyohusu masuala ya wanawake tunaweza kubadilisha vifungu.
Tuzungumzeni hoja tuache kufanya fujo, tusiingie katika malumbano
ambayo hayana tija, tuache kuzomea tukifanya hiyo tutakuwa tumejijengea
heshima,” alisema Mama Anne.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SPIKA ANNA MAKINDA ATOA DARASA KWA WANAWAKE KUCHANGIA HOJA ZA NGUVU KWENYE BUNGE LA KATIBA.”
Post a Comment