Friday, March 28, 2014
TUHUMA NZITO BUNGENI, NI ZA RUSHWA DHIDI YA WAZIRI MKUU PINDA.
Do you like this story?
Hali ya hewa jana ilichafuka kwenye Bunge la
Katiba baada ya mjumbe Ezekiel Wenje kuwatuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda na
baadhi ya mawaziri kuwa waliwahonga baadhi ya wajumbe wa kundi la 201.
Katika tuhuma hizo, Wenje alimtaja Waziri
Profesa Jumanne Maghembe, Dk. Shukuru Kawambwa na Gaudensia Kabaka akisema kuwa
walitoa rushwa ya vyakula, maji na vinywaji kwa wajumbe hao ili waunge mkono
msimamo wa serikali mbili.
Kauli hiyo, iliyotolewa katika mjadala wa
mabadiliko ya kanuni, ilisababisha mawaziri hao kunyanyuka kujibu tuhuma hizo,
huku Wenje akisisitiza kuwa aliyoyasema ni kweli tupu.
Vilevile baadhi ya wajumbe wanaotoka katika
kundi hilo walicharuka na kujaribu kujitetea huku mmojawapo akitishia kuwa
iwapo Wenje asingeomba radhi, asingetoka ndani ya Bunge hilo.
Wenje, ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana
(Chadema), alianza kwa kueleza kwamba wapinzani “walilia” sana kuwa Bunge la
Katiba lisingekuwa na usawa kutokana na Chama cha Mapinduzi kuwa na wajumbe
wengi, ndipo ikaonekana wapatikane wajumbe wengine 201, lakini jambo la ajabu
ni kwamba walioteuliwa katika kundi hilo asilimia 80 ni makada wa CCM akiwamo
mzee maarufu ambaye ameingizwa kama mganga wa jadi.
Ingawa hakumtaja jina, Wenje alikuwa
anamaanisha kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyeteuliwa kupitia
kundi la waganga wa jadi.
Kuhusu rushwa, Wenje alisema:“…Sasa kuna
wajumbe wa kundi la 201 walipelekwa kwa Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa
wamepeana rushwa, vikao vingi vilifanyika usiku. Hii haikubaliki.”
Baada ya kauli hiyo ya Wenje, Profesa
Maghembe alisimama ghafla huku akionekana kutaharuki, ambapo Makamu Mwenyekiti
Samia Suluhu Hassan alimpa nafasi ya kujieleza.
Profesa Maghembe alikiri kuwakaribisha baadhi
ya wajumbe wa kundi hilo, akieleza kwamba ilikuwa ni katika hali ya ukarimu
uliozoeleka miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
“Kuna kundi lipo hapa ambalo linafanya kazi
ya kudhalilisha wenzao. Ni kweli niliwaalika kwa chakula wajumbe hao kwa
taratibu za kawaida, lakini hakuna mbunge hapa anayeshindwa kujinunulia
chakula, hakuna anayeweza kupewa rushwa.
“Kwa sababu hiyo ninaomba kiti chako kimtake
mjumbe aliyewasilisha hoja hiyo aniombe radhi. Wenje aniombe radhi,” alisema
Profesa Maghembe akiwa katika hali ya hasira, huku kukiwa na sauti za kuzomea
na kushangilia kutoka kwa wajumbe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TUHUMA NZITO BUNGENI, NI ZA RUSHWA DHIDI YA WAZIRI MKUU PINDA.”
Post a Comment