Sunday, March 30, 2014
WAJUMBE WA BUNGE MAALUM WASUSIA BUNGE.
Do you like this story?
Wakati Bunge Maalumu la Katiba
linatarajia kuanza kujadili Rasimu ya Katiba kesho, baadhi ya wajumbe wa Bunge
hilo wameanza kuondoka bungeni, kupinga mwenendo wa Bunge hilo.
Hatua hiyo ya wabunge hao inakuja wakati
Bunge Maalumu la Katiba juzi lilipitisha azimio la kutumia kura ya siri na wazi
katika kuamua vifungu vya rasimu.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba,
Samia Saluhu alisema baada ya kupitishwa kwa utaratibu wa kupiga kura za siri
na wazi katika Bunge hilo, kuanzia Jumatatu wataanza kujadili sura ya kwanza na
sita ambayo inahusu Muundo wa Muungano.
Katika sura ya kwanza, mambo ambayo
yanatakiwa kujadiliwa ni Jina, Mipaka, Alama, Lugha na Tunu za Taifa wakati
sura ya sita mambo ambayo yanapaswa kujadiliwa ni Muundo wa Muungano.
Mjumbe wa Bunge hilo, Godbless Lema alisema
anakusudia kuondoka bungeni, kutokana na kutoridhishwa na maridhiano ya kupiga
kura za siri na wazi katika kufikia uamuzi katika Bunge hilo.
Akizungumza na Mwananchi jana, Lema alisema
hakubaliani na utaratibu uliopitishwa, kwani unalenga kulazimisha kila jambo
ambalo chama tawala kinalitaka lipitishwe.
“Huu utaratibu wa kura kupigwa kwa wazi na
siri katika kitu kimoja, haupo sehemu yoyote duniani. Sasa sisi kukubali ni
kuwasaliti wananchi, kwani hata Dodoma tunaandaa rasimu ya Katiba ya wananchi
wote siyo ya CCM pekee,” alisema Lema.
Amesema pia hakubaliani na utaratibu wa
kujadili rasimu ya Katiba, ambao umetolewa na Kamati ya Uongozi kwa kuanza na
sura ya kwanza na ya sita, kwani vinalenga kufumua Rasimu ya Jaji Warioba.
“Hapa CCM wanataka kulazimisha Serikali mbili
kwa kujadili kwanza vifungu hivi, kama vitapita basi watakuwa na uwezo wa
kubadili rasimu yote kitu ambacho mimi siwezi kukaa kwenye Bunge hili na
kusaliti wananchi waliotoa maoni kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa
na Jaji Joseph Warioba,” alisema Lema.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mjimkongwe,
Ismail Jussa, amesema uchaguzi wa vifungu hivyo ambavyo ndivyo vinabeba Rasimu
ya Katiba, vinaashiria kuvunjika kwa Bunge hilo katika hatua za awali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAJUMBE WA BUNGE MAALUM WASUSIA BUNGE.”
Post a Comment