Thursday, March 27, 2014
WALAGHAIWA KUSHIRIKI UKAHABA CHINA.
Do you like this story?
Serikali ya Tanzania imesema
kuwa imebaini kuwepo kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto wa kike kwenda
nchini China kwa lengo la kuwashirikisha katika ukahaba ambao unadaiwa
kusababisha kunyanyaswa kwa wasichana hao na wengine kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa
kimatifa nchini humo Bernard Membe amesema serikali itatuma wachunguzi nchini
Uchina kuchunguza biashara hiyo.
Hatua hiyo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya
msichana mmoja Mtanzania kuuawa kikatili katika mji wa Guangzhou nchini Uchina.
Waziri Membe amesema huenda baadhi ya
wahusika wa bishara hiyo ni Watanzania wanaosafirisha wasichana wa dogo kwa
kisingizio cha kuwatafutia ajira. Baadhi ya wanaosafirishwa hujipata pabaya
baada ya kuwasili Uchina ambapo hunyang'anywa hati zao za usafiri na
kulazimishwa kushiriki ukahaba.
Baadhi ya wakaazi wa Dar es laam
waliozungumza na BBC wameelezea kusikitishwa na vitendo hivyo na kuitaka
serikali ichukue hatua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WALAGHAIWA KUSHIRIKI UKAHABA CHINA.”
Post a Comment