Saturday, April 26, 2014

BUNGE MAALUM LA KATIBA LAAHIRISHWA HADI AGOSTI 5 MWAKA HUU, RAIS AONGEZA SIKU 60 TU.




Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba Mizengo Pinda (kushoto) na Mjumbe wa Bunge hilo Godfrey Zambi wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuhairishwa kwa Bunge hilo



Bunge  Maalumu  la  Katiba  limeahirishwa  leo  hadi  Agosti  5  mwaka  huu  ili  kupisha  bunge  la  Bajeti....Hii  ni  michango  ya    baadhi  ya  wajumbe  wa  bunge  hilo  kabla  ya  bunge  hilo  kuahirishwa...

Kingunge.
Nawashukuru sana waganga wa tiba asili kwa kunifanya nije hapa. Mimi nlikua mlezi wa chama hiki tangu 1998. Waliokua wanahoji walitaka watu waseme kwamba nimepenyapenya lakini mimi nimependekezwa na hiki chama. Ni chama cha heshima kwani kinatoa dawa za miti shamba sio ramli.

Haya mambo mliokua mnafanya ya kuzomea si sawasawa. kuna lugha zimetumika hazifanani na sisi wala Watanzania. Lugha za ugomvi na kudhalilisha.

Lugha za kudhalilisha waasisi wetu eti mwalimu Nyerere si Mungu je nani alikuambia ni Mungu?

Watu tumewasomesha . Swala kubwa la msomi ni unyenyekevu. Hapa tunapishana kwa mawazo tu. Hata rasimu hii ina mawazo tu, hakuna watu mle ndani ya rasimu.

Hapa hatuwazungumzi wajumbe wa timu, Warioba bali tunazungumzia haya mawazo yaliyo katika rasimu. Tuache kumshambulia Walioba. Chama changu CCM kina adabu sasa wewe unayemshambulia warioba unafedhehesha chama changu.

Mazungumzo tuliyo yafanya sura ya 1 na 6 tumefanya vizuri sababu maoni ya walio wengi na wachache yamejitokeza. Lakini kazi ya kufanya maamuzi bado.

Maoni yangu mimi; Sisi hapa tumetumwa na wananchi ili ipatikane katiba mpya iliyo bora sio ilimradi katiba.

Inabidi kwanza ijue katika miaka hii 50 tuna mafanikio makubwa kwa hiyo katiba bora lazima izingatie yale mazuli mfano Muungano wetu, Haya yote mafanikio yametokana na Muundo wa namna wake wa Serikali mbili.

Tunataka katiba itakayo punguza au kuondoa kero za Muungano, kama tutashindwa kuondoa hayo mapungufu itakua sio katiba bora. Naamini tutatumia kipindi hiki cha kupumzika kutafakari hili.

Tumeishi duniani na tumejifunza mambo. Katiba mpya lazima ilete mambo ya msingi na kuondoa hili kero la Umasikini uliokithili wa Nchi yetu. Mtaandika katiba lakini kama mtashindwa zungumzia Umasikini itakua sio katiba bora, Katiba mpya lazima izungumzie uchumi wa watanzania walio wengi.

Kupata katiba Mpya lazima kuwepo na maelewano humu ndani. Waliotoka nje walionyesha mapungufu makubwa lakini tunaomba warudi na wakirudi naomba tuelewane. Kupata theruthi mbili ya bara na zanzibar ni sheria.

Kule zanzibar kulilkuwepo na tatizo tangu mwaka 1998 limedumu kwa miaka 18 kila siku tunazungumza baadae tukaelewana tukazungumzi na Hamad rashid Nahodha mimi mwisho wa siku tukapata fomula maalim Seif sasa hivi ni Makamu Rais wa kwanza ni kutokana na Mazungumzo.

Sasa tuzungumze mpaka tuelewane na wakubwa nao inabidi wazungumze.Asante kwa kunivumilia may 30 ntafikisha miaka 82 si haba. asanteni sana
 
Kificho :
Mimi nimeshangaa sana watu wanaosema eti mimi naunga mkono serikali tatu, Tangu lini?

Mimi nasema naunga mkono serikali mbili ambazo zimedumisha Huu muungano wetu kwa miaka 50.
 
Balozi Seif Idd (makamu wa pili wa rais zanzibar):
Mimi naungana na walio wengi kwamba muungano wetu huu uwe wa walio serikali mbili. Wananchi wametuleta humu ili tuwapelekee katiba itakayokua kwa masirahi yao. Tumetumia gharama kubwa kutengeneza ukumbi huu ili tukae tustarehe lakini wenzetu wakaamua kutoka nje. Nawaomba warudi sababu katiba haitungwi Barabarani wala popote pale isipokua humu ndani tu.

Humu ndani kila mmoja nalipwa sh laki tatu kila siku tunayo kaa humu. kwa siku 70 tulizopangiwa tumetumia bil 20 mpaka sasa. Ndizo tulikua tutumie mpaka leo hii. Pesa nyingi zimetumika katika kutunga kanuni baada ya hapo kujadili siri au wazi. watu wakang'ang'ana sana kura ya siri. Lakini wale wale waliotaka kura za siri wakapiga wazi. uharibifu wa fedha.

Sura ya kwanza na ya sita tu ndo zimetumia bil 20. Leo tunaahilisha mpaka tarehe 5/8. Rais alikubali kuongeza siku 60 sasa tuangalie siku 60 tutatumia kiasi gani. Nia yetu humu ndani ya kutunga katiba. Watu wameshindwa kutunga katiba wameanza mwalimu nyerere... karume na kombo wakati hawawezi kuwajibu.

Mimi naomba wenzetu warudi waje tujadili katiba mpya ambayo wananchi wametutuma. Kero hizi za Muungano zinaweza kutekelezeka kwa muundo huu wa Muungano tulionao.  Nawasihi wenzetu walio toka warudi. asanteni.
 
Peter Pinda:
Mimi nilikua kamati namba moja. Nlikua nasikiliza mjadala huu kwa makini sana. tanzania ni miongoni mwa Nchi barani afarika ambayo tumeweza kuwa wamoja kutokana na muungano wetu ulio asisiwa na wasisi wetu. Mijadala iliyopita ilikua na vijembe na kejeli. Naishukuru kamati yako ya kanuni kwa kuendelea kuboresha kanuni hizi. Tunapokwenda tutajipanga vizuri zaidi.

Muungano wa Zanzibar na Tanganika umeelezwa na kuandikwa sana lakini ni vizuri tuendelee kuyaheshimu mawazo ya waasisi wetu wa Muungano.

Watu wanajaribu kulilia kitu ambacho hawajaexperience hata kidogo, nashangaa sana. Tanganyika imedumu mwaka mmoja na nusu lakini miaka 50 tupoTanzania. Tunaitaka Tanganyika Tanganyika ipi hyo?.

Mwalimu si mtu ambaye unaweza kumbeza kwa kiasi hicho kwani anaheshimika dunia nzima. Leo mtu anasimama kijana wa juzi anatumia lugha chafu kwa baba huyu! jamani.

Nikweli kero za muungano zipo. kweli muungano ulikua na kero 31 leo zimebaki 6. Ibara ya109 katika rasimu hii wameunda tume ya kushughulikia kero za Muungano. Nawashukuru sana tume ya Warioba kwa hili.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Hawa wenzetu waliotoka nawaomba kwa dhati kabisa warudi. Katiba yoyote kazi kubwa inayofanyika ni ya ujenzi wa katiba. Tuliwambia tuboreshe hii wakakataa eti wanataka mpya, mpya kwani ndo tunapata uhuru? sasa kipi kipya kilichoingia kwenye hii?.

Siafiki hata kidogo kwamba tume imetumia fedha nyingi kwa hiyo inabidi iletwe ya serikali tatu,  Watu wametazama takwimu wamehoji.
 
Wakati wa kuwasilisha wrasimu ya katiba limerudia sana kwamba ofisi ya waziri mkuu imependekeza serikali tatu. Mimi sikua ndani yake bali mimi nlitoa maoni yangu kama mimi. Na hii ya kutumia ofisi hizi mbili kupendekeza serikali tatu kwamba wananchi ndo wamependekeza hivyo sio sahihi hata kidogo.

Nawashukuru tume kwa kufanya kazi nzuri. Asanteni sana.

0 Responses to “ BUNGE MAALUM LA KATIBA LAAHIRISHWA HADI AGOSTI 5 MWAKA HUU, RAIS AONGEZA SIKU 60 TU.”

Post a Comment

More to Read