Friday, April 25, 2014
MOURINHO: NIACHIENI CHELSEA YANGU, KIKOSI SUBIRINI JUMAPILI.
Do you like this story?
JOSE Mourinho amegoma kuzungumzia
kuhusu kikosi atakachopanga katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England baina
ya klabu ya Chelsea dhidi ya Liverpool jumapili ya wiki hii katika dimba la
Anfield.
Siku za karibuni, Mreno huyo
alikaririwa akisema atapanga kikosi dhaifu katika mechi hiyo ili kuwapumzisha
wachezaji wake nyota kuelea nusu fainali ya pili ya ligi ya mabingwa barani
Ulaya dhidi ya Atlectico Madrid jumatano
ya wiki ijayo uwanja wa Stamford Bridge.
Mourinho alipoulizwa kuwa anaidharau
ligi ya England mpaka apange kikosi dhaifu?, kocha huyo, 51, alisema mambo ya
timu yake aachiwe yeye.
“Siku zote kuchagua kikosi
kitakachocheza ni siri ya kocha, Kama mtu anauliza swali hilo, siwezi kumjibu”.
“Kitu cha msingi ni klabu yangu na
mashabiki wetu. Nahita
ji kuilinda klabu na mashabiki wa
Chelsea”.
“Kama hatusaidiwi kutimiza ndoto zetu
na malengo yetu, basi kuna sababu ya kutuacha tufanye mambo yetu. Subirini
jumapili na mtajua timu itakayocheza” Alisema Mourinho.
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid
alipoulizwa kama mashabiki wa Chelsea watafurahishwa na mabadiliko ya kikosi,
alijibu kuwa mashabiki wa Stamford Bridge watakuwa na imani na maamuzi.
Mourinho alieleza kuwa leo hii hakuwa
huru katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia adhabu aliyopewa na chama
cha soka cha England, FA baada ya kumpongeza mwamuzi Mike Dean aliechezesha
mechi ya Chelsea dhidi ya Sunderland na kushuhudia paka weusi wakiibuka na
ushindi wa mabao 2-0.
FA wameyachukuliwa maneno ya Mourinho
kama kejeli, lakini yeye anachukuliwa kivingine.
Aliongeza: “Kila ninapozungumza kuna
madhara, hata kama nikisema mwamuzi amefanya kazi nzuri napewa adhabu, kwahiyo
sina uhuru kabisa. Kama mnataka mkutano mzuri nendeni mkazungumze na FA na sio
mimi”.
Pia Mourinho amethibitsiha kuwa nahodha
wake John Terry na mshambuliaji wake Eden Hazard watakosa mechi ya jumapili na
wapo hatarini kuwakosa Atletico
jumatano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MOURINHO: NIACHIENI CHELSEA YANGU, KIKOSI SUBIRINI JUMAPILI.”
Post a Comment