Friday, April 25, 2014
HII KALI: HUKO KENYA MWANANCHI ASIPOMUITA MBUNGE MHESHIMIWA NI KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA.
Do you like this story?
Wakenya wanakabiliwa na tisho la
kufungwa jela mwaka mmoja au kulipa faini ya dola 23,000 kwa kukosa kumuita
mbunge 'mheshimiwa' unapozungumza naye.
Sheria hii mpya inayopendekezwa na
wabunge wa Kenya inalenga kuhakikisha kila afisaa mkuu wa serikali anapewa
heshima anayostahili.Watakaovunja sheria hiyo watapata adhabu kali.
Adhabu hiyo itawakuta wale watakaokosa
kumpa Rais heshima zake kwa kumuita 'Mtukufu Rais', naye spika wa bunge
atapaswa kuitwa 'Mheshimiwa spika wa bunge'
Mswada huu uliwasilishwa na mbunge
mmoja kwa jina Adan Keynan, ambaye amesema kuwa umuhimu wake ni kuonyesha
heshima kwa maafisa wa serikali.
"ni muhimu kuonyesha picha nzuri
ya nchi, kuhakikisha kuna mpangilio na maadili mema katika mchakato wa utawala,
'' alisema bwana Keynan.
Huku mzozo kati ya wabunge na magavana
ukiendelea kutokota, mswada huo haujapendekeza chochote kuhusu cheo cha
magavana ambao ni wakuu wa majimbo na watakavyoitwa.
Wataendelea kuitwa tu magavana.
Wataendelea kuitwa tu magavana.
Mswada huo pia unapendekeza kuwepo vyeo
kwa maafisa wa serikali kulingana na ukubwa wao.
Ikiwa mswada huo utakuwa sheria, cheo cha mbunge kitakuwa juu zaidi kuliko cha gavana, majaji wa mahakama ya juu , marais wa zamani na makamu wa rais.
Kadhalika mswada huo utatumika katika kuweka mpangilio kuhusu ambavyo maafisa wa serikali watakuwa wanaketi katika hafla na mikutano ya serikali.
Maafisa wa serikali watakaojipatia vyeo vingine mbali na vile vitakavyoorodheshwa katika mswada huo watatowa faini ya dola milioni mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ HII KALI: HUKO KENYA MWANANCHI ASIPOMUITA MBUNGE MHESHIMIWA NI KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA.”
Post a Comment