Friday, April 25, 2014

OLE WAKO USITANGULIZE NENO “MHESHIMIWA KWA MBUNGE”


Bunge la Kenya


Mbunge wa Eldas Bw Adan Keynan





Utakuwa Hatarini kufungwa kifungo cha miezi 12 au kutozwa faini ya Shilingi 2 za Kenya kwa kukosa kumwita Mheshimiwa Mbunge ama utapata adhabu hiyo hiyo usipomwita Spika wa Bunge au Seneti 'Mheshimiwa  au Usipomuita 'Mtukufu’ Mkuu wa Nchi (Rais) wa Kenya.

Adhabu hiyo hiyo pia inakusubiri pia ukiamua kumwita Jaji wa Mahakama ya Juu kwa jina lake bila kumtambulisha kama 'Mheshimiwa Jaji’, Hii inatokana na Sheria mpya iliyopendekezwa kutoa mwelekeo kuhusu jinsi ya kutambua maafisa wa umma inapendekeza adhabu kali zaidi kwa watakaovunja sheria hizo.

Mswada huo ulioandaliwa na Mbunge wa Eldas Adan Keynan unasema mwongozo huo utaboresha sura ya kitaifa kwa kuhakikisha kuna mpangilio katika huduma za kitaifa.

“Nia kuu ya mswada huu ni kudumisha sura njema ya nchi, kudumisha mpangilio na nidhamu katika utawala,” mswada huo unaeleza, Huku Rais akitambuliwa kama 'Mtukufu’, naibu wake atatambuliwa kama 'Mtukufu Naibu Rais’ na Mama taifa ataitwa 'Mtukufu Mama Taifa’.

Huku makabiliano kati ya wabunge ambao sasa ni waheshimiwa, na mavana ukinukia, wakuu hao wa kaunti watakuwa wakitambuliwa tu kama 'Gavana’ huku ikipendekezwa jaji mkuu aitwe 'Mheshimiwa Jaji Mkuu’.

“Imenuiwa pia kutoa kigezo cha vyeo vinavyostahili kwa maafisa wote, ukuu wao na mpangilio wa ngazi za vyeo hivyo kwa minajili ya hafla za kitaifa,” mswada huo uliosomwa Alhamisi kwa mara ya kwanza ulieleza.

Mswada huo pia unapendekeza mpangilio wa vyeo ufuate ukuu wa maafisa wa umma, Katika mpangilio huo, wabunge ni wakuu kuliko magavana, majaji wa Mahakama ya Juu, marais na manaibu rais wa zamani, mawaziri, Mkuu wa Sheria na makatibu wa wizara.

Rais Uhuru Kenyatta ndiye aliye juu zaidi kwenye mpangilio huo, akifuatiwa na naibu wake William Ruto Wanaowafuata ni Spika Justin Muturi na Ekwee Ethuro ambao wamefuatwa na Jaji Mkuu. Wa tano katika mpangilio huo ni viongozi wa walio wengi na walio wachache katika bunge za Seneti na Kitaifa, kisha wabunge na maseneta ni wa sita na Magavana ni wa saba baada ya wabunge, kisha wamefuatwa na majaji wa Mahakama ya Juu.

Marais wa zamani Mwai Kibaki na Daniel arap Moi wako nafasi ya 10, huku waliokuwa Manaibu wao wakiwa katika nafasi ya 11, wakifuatwa na mabalozi Sheria hiyo itatumiwa kuandaa jinsi maafisa wakuu watakavyokuwa wakipangwa wakati wa hafla za kitaifa.

 

 

0 Responses to “OLE WAKO USITANGULIZE NENO “MHESHIMIWA KWA MBUNGE””

Post a Comment

More to Read