Tuesday, April 29, 2014
CECH, TERRY, ETO`O, HAZARD WAIPASHIA ATLETICO MADRID KESHO.
Do you like this story?
Petr Cech akitembea na Nathan Ake (katikati) na Marco van Ginkel kuelekea
katika mazoezi.
|
JOSE Mourinho ameanza maandaliza ya mechi
ya kesho ya nusu fainali ya pili ya UEFA dhidi ya Atletico Madrid, huku
ikishangaza kumuona mlinda mlango namba moja wa Chelsea, Petr Cech akifanya
mazoezi.
Cech aliteguka beka katika mchezo wa
kwanza uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana Vicente Calderon na Mourinho
alithibitisha wiki iliyopita kuwa kipa huyo anahitaji upasuaji ili kurudisha
bega katika hali yake
Nyota
wa samba: Willian, David Luiz, Ramires na
Oscar wakielekea katika uwanja wa Coham tayari kwa mazoezi.
Haikuwa rahisi kumouna Cech leo hii
ambaye alitakiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu, hivyo imeshangaza
kumuona mchezaji huyo akiwa miongozi kwa wachezaji waliofanya mazoezi leo hii.
Alipoulizwa kama yuko imara kwa mechi
ya kesho, alitabasamu na kusema “Ndiyo”, lakini alienda zake na kujiunga na
wenzake.
Cech alionekana akifanya mazoezi mepesi
leo hii, na makipa wenzake Mark Schwarzer, Henrique Hilario na Mitchell
Beeney walipoanza mazoezi na kocha wa
makipa, Christophe Lollichon, Cech
alikaa pembeni.
Mbali na Cech, wachezaji wengine
waliokuwa majeruhi, Samuel Eto`o, nahodha, John Terry, na Eden Hazard nao
wamefanya mazoezi leo hii kujiandaa na kipute cha kesho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CECH, TERRY, ETO`O, HAZARD WAIPASHIA ATLETICO MADRID KESHO.”
Post a Comment