Tuesday, April 29, 2014
DILI LIMEKAMILIKA! DIDIER KAVUMBAGU AMWAGA WINO AZAM FC.
Do you like this story?
DIDIER Kavumbagu kwaheri Yanga. Hii ni
baada ya mchana wa leo kusaini mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa wapya wa ligi
kuu soka Tanzania bara, klabu ya Azam fc, lakini kuna kipengele kinachosema
ataongezewa mwaka mwingine kama atafanya kazi nzuri.
Taarifa hii imethibitishwa na meneja wa
Azam fc, wana Lambalamba, Jemedari Said.
“Kavumbagu is a done deal! Tumemalizana
nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja, so tutakuwa nae msimu ujao kwenye
kampeni ya kutetea ubingwa wetu pamoja na michuano ya klabu bingwa ya Afrika,”
alifunguka Jemedari
Mshambuliaji huyo hatari na nahodha wa
timu ya Taifa ya Burundi ameamua kumwaga wino Azam baada ya Uongozi wa Yanga
kusuasua kumpa mkataba mwingine baada ya ule wa miaka miwili kumalizika.
Kavumbagu mara kadhaa alikaririwa na
vyombo vya habari kuhitaji mkataba mpya katika klabu ya Yanga, lakini viongozi
wa kalbu hiyo hawakuonesha nia na leo hii imeamua kuanza maisha mapya Chamazi.
Katika maelezo yake, Kavumbagu alieleza
kuwa mpira ni sehemu ya maisha yake na kazi yake, hivyo yuko tayari kuichezea
klabu yoyote yenye nia ya kumsajili kwa masharti ya kukidhi mahitaji yake ya
msingi.
Azam fc wenye nia ya kufanya vizuri
katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani, wamekusudia kuongeza
nguvu katika kikosi chao.
Kocha mkuu, Mcameroon, Joseph Marius
Omog ameenda likizo kwao Cameroon , lakini uongozi wa Azam ulithibitisha
kupokea taarifa ya mapendekezo yake na tathimini ya msimu uliomalizika aprili
19 mwaka huu.
Usajili huu unathibitisha kuwa
Kavumbagu alikuwa katika rada za Omog na aliwaachia viongozi mpango mzima.
Kuzugazuga kwa Uongozi wa Yanga
kumemfanya nyota huyo kuangukia mikononi mwa matajiri wa Azam fc japokuwa
alikuwa tayari kumwaga wino tena katika klabu ya Yanga.
Mkataba aliosaini Azam fc unasemekana
kuwa na masilahi bora zaidi ya ule wa Yanga.
Nyota huyo mwenye uchu wa mabao
alijiunga na Yanga mwaka 2013 akitokea klabu ya Atletico ya nchini Burundi.
Kavumbagu amesaini mbele ya Katibu Mkuu
wa klabu ya Azam, Nassor Idrisa makao makuu ya klabu, Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.
Nassor amekaiririwa na Tovuti ya klabu
akisema; “Tumepata mshambuliaji mzuri, ambaye tayari ana uzoefu wa kucheza Ligi
Kuu ya Tanzania kwa misimu miwili, mchezaji huyu ni chaguo la kocha wetu Joseph
Omog, ambaye alivutiwa naye baada ya kumuona akichezea klabu yake zamani, Yanga
SC,”alisema.
Kwa upande wake, Kavumbangu ameiambia
Tovuti ya Azam kuwa; “Mimi ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba
Yanga, lakini viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua
kusaini,”.
Mshambuliaji huyo mrefu mwenye nguvu
amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri wake mpya, Azam FC ambako pia
amepania kwenda kushinda mataji na kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said
Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.
“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam,
nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu huwa nashabikia klabu
nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa Azam,”amesema.
Kavumbangu alitua Yanga mwaka 2013
akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi misimu miwili ya kuichezea klabu
hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote, moja tu la penalti.
Kila la heri Kavumbagu katika maisha
mapya Azam fc.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DILI LIMEKAMILIKA! DIDIER KAVUMBAGU AMWAGA WINO AZAM FC.”
Post a Comment