Tuesday, April 29, 2014
MATOGOLO WA MBEYA CITY AFUNGUA MILANGO KWA AZAM, SIMBA, YANGA…..
Do you like this story?
Antony Matogolo mwenye jezi namba 16 mgongoni wakati wa mechi yao na Azam fc uwanja wa sokoine jijini Mbeya
|
CHAMA cha soka mkoani Mbeya, MREFA,
kimeendelea kujivunia mafanikio ya kuaminiwa na shirikisho la soka Tanzania TFF
kwa kuziweka timu za Taifa mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa MREFA, Elias Mwanjala
ameuambia mtandao huu kuwa kuwekwa kambi ya maboresho ya Taifa stars mjini
Tukuyu ilikuwa fursa nzuri kwa wafanyabiashara na wapenzi wa soka mkoani humo
kuiona timu yao.
Mwanjala aliushukuru uongozi wa TFF
chini ya rais Jamal Malinzi kwa kuendelea kuwapa fursa muhimu kama hizo na hasa
baada ya kuamua mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Taifa Stars na Malawi
kufanyika mkoni humo.
“TFF wanajua juhudi zetu. Uwanja wa
Sokoine ulikuwa mbaya sana, lakini tumeuboresha kwa nguvu zote na sasa mechi ya
kirafiki ya Taifa stars inafanyika katika uwanja huu. Hii ni heshima kubwa kwa
MREFA”.
“Kwasasa tunajenga vyumba vya
kubadilishia nguo vyenye hadhi ya kimataifa. Dhamira yetu ni kuwa na uwanja
bora zaidi weye hadhi kubwa”. Alisema Mwanjala.
Taifa
stars chini ya Kocha mpya, Mart Nooij aliongeza wachezaji tisa katika kikosi
kilichochapwa mabao 3-0 na Burundi siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano
wa Tanganyika na Zanzibara, aprili 26 mwaka huu uwanja wa Taifa.
Wachezaji
hao waliongezwa kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi (The Flames)
itakayochezwa Mei 4 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Wachezaji
walioongezwa ni Edward Charles Manyama (JKT Ruvu), Elias Maguli (Ruvu
Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam),
Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari
Kapombe (AC Cannes, Ufaransa).
Kwasasa Stars ipo kambini mjini Tukuyu
na siku mbili kabla ya mechi hiyo itarudi mjini Mbeya tayari kwa maandalizi ya
mwisho.
Akizungumzia timu za Prisons na Mbeya City
fc, Mwanjala alisema zimejitahidi kupambana msimu uliopita wa ligi kuu ingawa
zimeishia maeneo tofauti.
“Mbeya City tulianza kupotea baada ya
kufungwa na Yanga, Coastal na mwisho Azam fc”.
“Timu haikuwa na uzoefu, lakini msimu
ujao tutakuwa mabingwa kwasababu tutakuwa wazoefu”.
“Kwa Prisons kidogo uzoefu mdogo
walionao umewabakisha ligi kuu, kikubwa ni kuziandaa timu hizi ili msimu ujao
zifike mbali”.
“Prisons ilipoteza kete zake mzunguko
wa kwanza, lakini raundi ya pili ilicheza soka zuri sema bahati haikuwa yao.”
Alisema Mwanjala.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa
wanajitahidi kuisaidia timu nyingine ya Kimondo fc ili iingie ligi kuu.
“Tuna imani Kimondo fc itaweza kupanda ligi
kuu, lakini kumbuka tuna timu nyingie ya Wenda fc, mabingwa wa mikoa”
“Wanaenda kushiriki ligi ya mabingwa wa mikoa,
tunaamini itafuzu kucheza ligi daraja la
kwanza”. Aliongeza Mwanjala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MATOGOLO WA MBEYA CITY AFUNGUA MILANGO KWA AZAM, SIMBA, YANGA….. ”
Post a Comment