Tuesday, April 8, 2014
MTENDAJI WA KIJIJI AKAMATWA MKUTANONI KWA WIZI WA MIFUKO 189 YA MBOLEA YA RUZUKU.
Do you like this story?
Mtendaji wa Kijiji cha Iwiji Kata ya Iwiji Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya Anthon Ndisa akielekea kupanda gari ya polisi baada ya kutuhumiwa kuiba mifuko 189 ya mbolea ya ruzuku |
Mtendaji wa Kijiji cha Iwiji Kata ya
Iwiji Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya Anthon Ndisa anashikiliwa na Jeshi la Polisi
kuhusiana na upotevu wa Mbolea za ruzuku mifuko 189 kwa kipindi cha mwaka
2013/2014.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed
Msangi amethibitisha kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Iwiji na kumtuma
Mkuu wa Polisi wilaya ya Mbeya Richard Mchomvu ili kujua hatma ya suala hilo.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika
Kijijini hapo na kuhudhuriwa na Afisa tarafa Sote ambapo Afisa Kilimo Maserlin
Mlelwa alitoa takwimu za mgao wa mbolea kwa kijiji hicho na utaratibu
uliotakiwa kufuatwa kugawa mifuko hiyo 189.
Ndisa alipotakiwa kujieleza katika
mkutano huo amedai kuwa alilazimika kuwatumia wenyeviti wa vitongoji kutokana
na kamati ya mbolea ya kijiji kuvunjwa na wananchi hao jambo ambalo wananchi
walilipinga.
Mbolea hiyo imetolewa na Serikali
Mwishonni mwa mwaka jana lakini imedaiwa mbolea hiyo haikuwafikia walengwa na
kuleta malalamiko kijijini lawama kubwa ikielekezwa kwa mtendaji wa kijiji
Anthon Ndisa aliyepewa dhamana ya kusimamia ugawaji wa pembejeo hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya
ya Mbeya Richard Mchovu amesema kuna taratibu za kiutawala zilikiukwa hivyo
watafungua jalada la uchunguzi kwa mtendaji wa kijiji hicho na kumpatia mwajiri
wake ambaye ni Mkurugenzi wa Wilaya na ikithibitika hatua za kinidhamu
zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Mkutano huo pia ulimtupia lawama Diwani
wa Kata hiyo Anderson Kabenga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mbeya kwa kufumbia macho kero za wananchi licha ya kupewa taarifa mara kwa
mara.
Aidha wananchi hao walikerwa na kitendo
cha mtendaji kuwakamata wananchi waliokuwa wakifuatilia mgao wa mbolea kwa
madai ya kumtishia kuuawa tukio lililofanyika Mwezi Februari mwaka huu na
kwenda Polisi Kituo cha Ileje badala ya Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTENDAJI WA KIJIJI AKAMATWA MKUTANONI KWA WIZI WA MIFUKO 189 YA MBOLEA YA RUZUKU.”
Post a Comment