Monday, April 28, 2014

RAIS MSTAAFU WA KENYA AZUSHIWA KIFO NA MITANDAO YA KIJAMII.


Kumekuwepo taarifa zilizozagaa kwenye baadhi ya mitandao mingi ya kijamii, zikidai kuwa rais wa awamu ya Pili wa Kenya Mh. Daniel Arap Moi kuwa amefariki dunia akipatiwa matibabu

Mtandao huu umewasiliana na mwanahabari Julius Kipkoech kutoka nchini Kenya ambaye amesema taarifa hizo si za kweli na hakuna rais wa Kenya aliyefariki zaidi ya mwasisi wa taifa hilo marehemu Jomo Kenyatta

Cha kushangaza ni kwamba taarifa hizo zimezagaa toka jana, lakini hakuna vyombo vikubwa vya habari vya ndani na nje ya Kenya vilivyoripoti habari hiyo unayomuhusu aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa wa Kenya hadi alipostaafu, ajambo lililopelekea mtandao huu wa www.eddymoblaze.blogspot.com kutaka kufahamu kulikoni na ukweli wa taarifa hizo ambazo si sahihi ama ni uzushi tu.

"Hakuna Rais amefariki Kenya isipokuwa Rais Mwazilishi Mzee Jomo Kenyatta" amesema mwanahabari Julius Kipkoech

0 Responses to “RAIS MSTAAFU WA KENYA AZUSHIWA KIFO NA MITANDAO YA KIJAMII.”

Post a Comment

More to Read