Monday, April 28, 2014

WAALIMU WALALA MADARASANI HUKO SHINYANGA, SHULE HAINA VYOO....!!!!!.




WAANDISHI wa habari nchini wanatarajiwa kuungana na wenzao duniani katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD), yanayotarajiwa kufanyika Mei 2-3.

Akitangaza sherehe hizo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Taasisi ya  Vyombo vya habari Kusini mwa Jangwa la Sahara (MISA), Mohammed Tibanyendera, alisema maadhimisho hayo yatakayowashirikisha washiriki zaidi ya 200 yatafanyika jijini Arusha.

Alisema sababu za maadhimisho hayo kufanyika Arusha ni kupata mrejesho wa maazimio waliyoyafikia kwa kuyapatia kaulimbiu ya “Mount Meru Declaration”.

Alibainisha baadhi ya mambo waliyokubaliana katika maadhimisho kama hayo mwaka jana yaliyozishirikisha nchi jirani, ni pamoja na kuboresha hali za wanahabari.

Tibanyendera alisema katika sherehe hizo kunatarajiwa kuzinduliwa machapisho mbalimbali, ikiwamo ripoti ya hali ya vyombo vya habari Tanzania 2014.

Ripoti nyingine itakuwa utafiti wa vyombo vya habari 2014 na ripoti ya uvunjifu wa uhuru wa vyombo vya habari kwa mwaka 2014.

Alisema katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa aliyekuwa Jaji Mkuu na Mwanasheria, Mark Bomani.

0 Responses to “WAALIMU WALALA MADARASANI HUKO SHINYANGA, SHULE HAINA VYOO....!!!!!.”

Post a Comment

More to Read