Wednesday, April 30, 2014
STEVEN MAZANDA: BADO NINA DENI NA MBEYA CITY FC, AFYA YANGU INAIMARIKA.
Do you like this story?
KIUNGO matata wa Mbeya City fc, Steven
Mazanda ataendelea kuitumikia klabu yake hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka
Tanzania bara kutokana na kubakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake.
Mazanda ameuambia mtandao huu kuwa bado
anadaiwa na klabu yake na kwa bahati mbaya malengo yake hayakutimia msimu
uliopita baada ya kuishia nafasi ya tatu
katika msimamo.
“Kitu kikubwa ni maslahi. Lakini
sidhani kama Mbeya City watashindwa kunipa kile ninachohitaji”.
“Nimesikitishwa sana na timu yangu kushika
nafasi ya tatu. Tulikuwa na malengo ya ubingwa, lakini haijatokea”.
“Mechi zote za mwisho sikucheza
kwasababu ya majeruhi ya mguu wangu wa kulia, nadhani nitakuwepo msimu ujao
kuendeleza harakati”. Alibainisha Mazanda.
Hata hivyo, Mazanda aliongeza kuwa
kwasasa anaendelea kujitibu mguu wake wakati huu wa likizo.
“Ninaendelea na matibabu ya mguu wangu.
Hali sio mbaya kwasasa kwasababu napiga mazoezi mepesi mepesi ili kujiimarisha
afya yangu”. Alisema Mazanda.
Mazanda ambaye ni chaguo la kwanza
katika nafasi ya kiungo namba nane kwa kocha Juma Mwambusi hakusita kuwashauri
vijana wa Mbeya City fc kuwa maslahi ni kitu cha kwanza katika mpira, lakini
waangalie sana aina ya timu zinazowahitaji.
“Unaweza kutoka Mbeya City ukaenda
klabu nyingine kwa kufuata maslahi, lakini ukakosa nafasi ya kucheza”
“ Ni vizuri kufikiria vizuri unapoamua
kuondoka ili usije kumaliza soka lako”.
“Siogopi kucheza timu nyingine
kwasababu ukijituma unapata namba. Cha msingi tujipange vizuri”. Alisema
Mazanda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “STEVEN MAZANDA: BADO NINA DENI NA MBEYA CITY FC, AFYA YANGU INAIMARIKA.”
Post a Comment