Tuesday, April 1, 2014

WAFYEKA MBUZI 15 WA M/KITI WA KIJIJI.


Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi




Watu wasiofahamika wamebomoa nyumba na kuwaua mbuzi 15 wa mwenyekiti wa Kijiji cha Usoke Wilaya ya Momba mkoani hapa, Stanslaus Simwiche.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema mbuzi hao waliuawa kwa kukatwa kwa mapanga usiku wa kuamkia jana.
“Mbali ya kufyeka mbuzi, watu hao pia walibomoa nyumba na kuharibu mali mbalimbali ambazo ujumla zina thamani ya Sh5.6 milioni.’’

Msangi alisema polisi wanachunguza tukio hilo, lakini taarifa za awali zinadai kwamba watu hao waliua mbuzi hao kutokana na mgogoro wa kijamii unaohusishwa na imani za ushirikina.

Alisema baadhi ya watu walikuwa wakimtuhumu mwenyekiti huyo kuwa mshirikina baada ya kifo cha mtu aliyefahamika kwa jina la Frank Abeid aliyefariki Machi 27 katika Kijiji cha Tusulu.
Kamanda Msangi alisema kutokana na tukio hilo, msako wa polisi umeanza ili kuweza kuwakamata wahalifu hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Kamanda Msangi alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuendeleza vitendo vya kuvunja amani.

0 Responses to “WAFYEKA MBUZI 15 WA M/KITI WA KIJIJI.”

Post a Comment

More to Read