Thursday, April 2, 2015

MAMA AWAFUNGIA NDANI WATOTO WAKE 3 KWA MIAKA 10 HUKO MAFIA!




Katika Kisiwa cha Mafia mkoa wa Pwani mama aitwaye Mwasiti Ally amekuwa akiwafungia ndani watoto wake ndani kwa muda wa miaka 10 sasa kwa madai kuwa ni wagonjwa wa akili.

Watoto hao huko ndani ya chumba wote wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku kucha za mikononi na miguuni kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi cha kutisha na sura zao kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu.

Alianza kuugua mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa, cha ajabu, kila mwaka mwingine akafuatia hadi wa tatu. Mama huyo anadai Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 anasema ni kwaajili ya usalama wao maana anaamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.

0 Responses to “MAMA AWAFUNGIA NDANI WATOTO WAKE 3 KWA MIAKA 10 HUKO MAFIA!”

Post a Comment

More to Read