Wednesday, April 1, 2015
SIMBA YAULA YAINGIA MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA EAG GROUP L.T.D
Do you like this story?
Rais wa Simba Evans Aveva na mkurugenzi mtendaji wa Eag Group Imani Kajula wakitia saini mkataba huo |
Rais wa simba na mkurugenzi mtendaji wa Eag Group wakikabidhiana mkataba baada ya kusaini |
Mkurugenzi mtendaji wa Eag Group Imani Kajula akiwa na wakurugenzi wa kibiashara wa Arsenal ambao wameingia mkataba na kampuni hiyo |
Kampuni ya EAG Group Limited,
imeingia mkataba wa miaka mitano na klabu Simba kwa ajili ya kuitafutia mipango
thabiti ya kuiendesha timu hiyo kuhakikisha inapiga hatua katika maendeleo
yake.
EAG Group iliingia mkataba na timu
hiyo leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun iliyopo Posta jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na FAHARI NEWS , Rais wa
Simba, Evans Aveva alisema kuwa kwa kumpitia udhamini wa kampuni hiyo wameandaa
tuzo mbalimbali kwa wachezaji wao kuhakikisha wanajituma uwanjani.
Aveva alizitaja tuzo hizo ni ya
mchezaji bora wa mwaka atakayepewa gari jipya, mchezaji kijana mwenye kipaji
atkayepewa milioni 5 na mchezaji mwenye nidhamu atakayeramba milioni moja.
Pia, wachezaji hao wote kila mmoja
atapewa zawadi ya simu aina ya Huawei yenye thamani ya shilingi milioni moja
ambao nao wameingia kwenye udhamini huo.
“Lengo tunataka kuona timu yetu
inapiga hatua katika soka ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika Mashariki na
Kati na ndiyo tumetoa zawadi hizo kwa ajili ya kuwapa morali wachezaji wetu
kupitia Kampuni ya EAG Group Limited na Huawei,” alisema Aveva.
Pia Mkurugenzi wa kampuni ya EAG
Group, Imani Kajula alisema kuwa, huo ndiyo wa udhamini kwao, wamepanga kuleta
mabadiliko ya soka kwa kuhakikisha wanawekeza zaidi kwa vijana kwa kuanza na
Simba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMBA YAULA YAINGIA MKATABA MNONO NA KAMPUNI YA EAG GROUP L.T.D ”
Post a Comment