Wednesday, April 1, 2015
MANGU APANGA NA KUPANGUA MAKAMANDA WA POLISI NCHINI.
Do you like this story?
Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu
amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa mbalimbali
nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji
wa Jeshi la Polisi Advera Bulimba alisema kwamba miongoni mwa makamanda wa mikoa
waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu
Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa
wa Mwanza na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa
afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna
wa Intelijensia makao makuu. Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Naibu
Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa mkuu wa
polisi jamii na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha
ufundi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya.
Wengine ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa
wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Kamwela
amehamishiwa Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fulgence
Ngonjani.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei amehamishiwa Kanda
Maalum ya Dar es Salaam kuwa mkuu wa utawala na nafasi yake kuchukuliwa na
aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Jafary Mohamed.
Aidha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Ferdinand Mtui aliyekuwa mkuu wa operesheni maalum polisi makao makuu
ameenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma.
Zaidi ya hao wengine waliohamishwa ni pamoja
na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) Frasser Kashai amehamishiwa Polisi makao makuu na nafasi yake
kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP) Zuberi Mwombeji.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kihenya Kihenya amehamishiwa polisi makao
makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya ya kati
Ilala, Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Satta.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi hilo
limesisitiza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida katika kuhakikisha kwamba
usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MANGU APANGA NA KUPANGUA MAKAMANDA WA POLISI NCHINI.”
Post a Comment