Tuesday, April 8, 2014
WAJUMBE WAKIMBILIA USAFIRI WA BODA BODA.
Do you like this story?
Baadhi ya
wajumbe wa bunge la katiba wameamua kutumia usafiri wa pikipiki katika mizunguko yao mjini Dodoma, ikiwa ni miongoni mwa hatua za kupunguza ghalama.
wajumbe
kadhaa kutoka kundi la 201 wakiwa
katika mizunguko ndani ya mji wa Dodoma kwa kutumia
usafiri wa pikipiki.
Ghalama za teksi kwa safari za katikati ya mji ni sh 3,000
wakati pikipiki ni sh 1,500 hadi sh 1,000 kulingana na mapatano kati ya abilia
na mwendesha pikipiki.
Kutokana na
uwamuzi huo, madereva teksi wamekuwa
wakilalamikia kutoona tofauti ya mapato
kwa siku kati ya Bunge la katiba na Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
‘’Matumaini
yetu ni kufanya Biashara kubwa wakati huu wa Bunge la katiba,
lakini hali imekuwa sawa tu na Bunge la Jamuhuri ya muungano,’’ alisema dereva
teksi, Said Yasin.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAJUMBE WAKIMBILIA USAFIRI WA BODA BODA.”
Post a Comment