Tuesday, April 8, 2014
WAZANZIBAR ‘WAMKUNA’ MTIKILA.
Do you like this story?
Dodoma. Mjumbe wa Bunge la katiba,
Mchungaji Christopha Mtikila amewapongeza
Wajumbe kutoka Zanzibari kwa kutetea haki za Watanganyika.
Mchungaji Mtikila alisema, chini
ya mwenyekiti Ole Sendeka, wajumbe wa
kamati hiyo walikataa mapendekezo mengi
yaliyolenga kubadili baadhi ya
vipengele vya sura ya kwanza na sita na
kusababisha kukosekana thelathini mbili
ya kula kwa upande wa Zanzibar.
Alisema hiyo inamaanisha mfumo wa rasimu iliyowasilishwa bungeni na kuanza kuboreshwa na Bunge hilo Jumatatu,
haukuathiliwa na uamuzi ya kamati hiyo.
‘’Raha niliyoipata kwa Ole Sendeka ni
kupewa nafasi ya kuzungumza, nikaitumia kuwafundisha Wajumbe hasa Watanganyika
Wenzangu kujitambua na kuthamini
utaifa Wao,’’ alieleza
Mchungaji Mtikila.
Alisema kujitambua na kuifadhi
historia ya asili na utaifa wa mtu ni mpango wa uumbaji wa Mungu, ambao
hautakiwi kuzuiwa na yeyote kwa sababu
yeyote na kwamba anayelazimisha kuhalibu mpango ni shetani.
Alisisitiza kuwa mchakato wa katiba
umethibitishia ulimwengu kuwa
Wazanzibari wanajitambua. Wanathamini utu na utaifa wao tofauti na
watanganyika.
‘’Roho ya uhanga kwa ajili ya kabila, ukoo, jamii au taifa lake imeumbwa
na Mungu ndani ya kila mwanadamu na
kuzuia utendaji wake ni dhambi . Hivyo Watanganyika nao lazima Wafuate nyayo za Wazanzizar katika
hilo,’’alieleza Mchungaji Mtikila.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAZANZIBAR ‘WAMKUNA’ MTIKILA.”
Post a Comment