Tuesday, April 8, 2014
WABADILI MBINU KUSAFIRISHA ‘UNGA’.
Do you like this story?
Dar es
salaamu. Wakati kitendo cha kudhibiti Dawa za kulevya Tanzania kikiumiza kichwa
ni namna gani kitamaliza wimbi la
biashara na matumizi ya dawa za kulevya, wahalifu wamegundua njia mpya za
kusafirisha kilevi hicho ikiwamo kuwatumia wanawake wajawazito.
Imeelezwa
kwamba mbali ya kuwatumia wajawazito. Pia hutumia ndege za mizigo kwa kuweka
dawa za kulevya kwenye wanasesere au jarida,makopo ya maziwa ya watoto, vinyago
na kuzituma kama vifurushi kwenda sehemu nyingine.
Akizungumza
jana, kamanda wa kitengo hicho Godfrey Nzowa amesema wasafirishaji hao wanawatumia wajawazito kwa sababu wanawaamini
kuwa hawawezi kukaguliwa kwa mashine kutokana na sababu za kiafya.
Alisema hali
imekuwa ikiwapa wakati mgumu kuwabaini wajawazito wahalifu wanapofika kwenye
viwanja vya ndege kwa kuwa hawakaguliwi kwa mashine hizo.
‘’Mwaka 2012
tuliwakamata wajawazito wakiwa wmemeza dawa za kulevya na hadi sasa tunaendelea
kuwakamata kwa kupata taarifa kutoka kwenye mataifa tunayo shirikiana nayo katika
kupambana na dawa za kulevya,alisema na kuongeza:” kama hatujapata taarifa,
mjamzito huyo anapitisha dawa za kulevya kwa sababu hakaguliwi na mashine za
X-ray kwa ajili ya kumlinda mtoto aliye
tumboni nah ii ni changamoto kubwa sana,”alisema kamanda Nzowa.
Alisema njia
nyingine ni kusafirisha dawa aina ya Cocaine kwa kutumia mfumo wa maji. Alisema
wahalifu hao wamekuwa wakisafirisha dawa hizo kwa kuziweka kwenye makontena
huku zikiwa kwenye madumu na chupa wakidai kuwa ni maji.
Alisema njia
nyingine inayotumika hivi sasa ni ya watoto wadogo… ‘’Mfano mtuhumiwa
aliyekamatwa hivi karibuni na kilo 3.6 za Cocaine alimtanguliza mtoto wake wa
miaka saba akidai anakwenda uturukikwa mumewe kumpeleka mwanaye,’’ alisema
kamanda Nzowa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WABADILI MBINU KUSAFIRISHA ‘UNGA’.”
Post a Comment