Tuesday, April 8, 2014
MAJAMBAZI YAUA, YATEKA MAGARI YA MAGAZETI.
Do you like this story?
Morogoro. Mtu mmoja amefariki dunia
na wengine 19 kujeruhiwa kwa kukatwa mapanga na kupigwa na kundi la watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi
Ambao walifunga Barabara ya morogoro-
iringa,eneo la mkata, Doman a kuteka magari kisha kupora mali na fedha za
wasafiri.
Miongoni mwa magari yaliotekwa,limo
la kampuniya Mwananchi
Lililokuwa likisafirisha
magazeti kwenda mikoa ya iringa na mbeya
na jingine la kampuni ya Global
Publishers ambalo nalo lilikuwa likisafirisha magazeti.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa
mor
ogoro, John laswai alisema tukio hilo
la utekaji lilitokea juzi usiku kati ya saa saba na saa tisa usiku. Aliyefariki
katika tukio hilo ni Alex Mgombea (38)
ambaye alizama kwenye mto uliopo jirani na eneo hilo wakati majambazi hayo yalipokuwa yakimfukuza kwa mapanga na silaha nyingine.
Kaimu kamanda huyo amesema majeruhi
wa tukio hilo wamelazwa katika hospitali ya rufaa mkoani morogoro na hali zao
zinaendelea kuimalika.
Hata hivyo. Alisema hakuna
aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kwamba jeshi la polisi
linaendelea na uchunguzi zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAJAMBAZI YAUA, YATEKA MAGARI YA MAGAZETI.”
Post a Comment