Sunday, August 14, 2016
FIFA KUFUNGA DIRISHA LA USAJILI LEO, TIMU ZATOZWA FAINI
Do you like this story?
Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), leo saa 6:00 usiku litafunga tena dirisha
la usajili baada ya kulifungua jana kwa saa 48 na imebainika kuwa timu tatu
zaidi zilikuwa na dosari katika usajili hivyo kufanya ongezeko la kutoka timu
nane zilionekana kwa haraka mapema wiki hii mara baada ya dirisha kufungwa
Agosti 6, 2016.
Timu hizo kwa ujumla
zilikuwa na dosari ya ama kutokusajili kabisa au kutokamilisha usajili wa
ushiriki wa ndani kwa msimu wa 2016/2-17. Timu tatu nyingine zilizobainika leo
Agosti 14, 2016 katika mtandao ni pamoja na Toto African ya Mwanza na Stand
United ya Ligi Kuu Tanzania Bara kadhalika Arusha FC ya Arusha ambayo msimu huu
itashiriki Ligi Daraja la Pili (SDL).
Hadi tunatuma taarifa
hii usajili ulikuwa ukiendelea kwa mfumo wa mtandao (TMS) ikiwa na maana ya
Transfer Matching System, lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
limerejea kanuni za usajili hivyo kuzitoza faini timu zilizokuwa na dosari.
Faini imetozwa kwa viwango tofauti kulingana na mashindano.
Timu zinazohusika na
usajili wa mtandao ni zile zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL), Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes (SFDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL)
na adhabu ya kushuka daraja na kwenda kushiriki Ligi ya Wilaya kisha Ligi ya
Mabingwa Mikoa (RCL) ambayo usajili wake ni wa kutumia karatasi.
Timu za Ligi Kuu
ambazo zilikatiwa mawasiliano baada ya kushindwa kuwahi tarehe ya mwisho ya
usajili ni Young Africans ambayo haikusajili kabisa. Kwa kufanya makosa hayo,
kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom, Young Africans imeadhibiwa faini
ya shilingi milioni tatu (Sh. 3,000,0000). Young Africans imetozwa faini hiyo
kwa kutosajili jina hata moja kabla ya Agosti 6, 2016.
Timu nyingine za Ligi
Kuu ambazo hazikukamilisha usajili angalau kufikisha wachezaji 18 ni African
Lyon ya Dar es Salaam, Stand United ya Shinyanga na Toto African ya Mwanza
ambazo kila timu imetozwa faini ya shilingi milioni moja (Sh.1,000,000).
Kwa timu za Daraja la
Kwanza la StarTimes (SFDL), Coastal Union ya Tanga pekee imetozwa faini ya
shilingi milioni moja (Sh.1,000,000) wakati timu nyingine za daraja hilo,
Kiluvya United na Friends Rangers za Dar es Salaam pamoja nna Panone, zimetoswa
faini ya shilingi laki tano (Sh. 500,000) kila moja.
Kadhalika kwa timu za
Daraja la Pili (SDL), ambazo ni Kitayose ya Kilimanjaro, Mashujaa ya Kigoma na
Arusha FC ya Arusha, zimetozwa faini ya shilingi laki tano (Sh. 300,000) kila moja.
Faini hiyo ni kwa timu na uongozi husika hauna budi kuilipa mara moja, kwani
TFF haitatoa leseni za wachezaji kama timu haijalipwa faini hiyo.
Kanuni
zinazozungumzia usajili ni Sura ya 10 inayozungumzia usajili na 11
inayozungumzia Adhabu Zihusuzo Usajili Na Uhamisho kadhalika Uhamisho Nje ya
Nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ FIFA KUFUNGA DIRISHA LA USAJILI LEO, TIMU ZATOZWA FAINI”
Post a Comment