Tuesday, August 16, 2016
WATU WATANO AKIWEMO ASKARI WA JWTZ WATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUTENGENEZA VYETI FEKI.
Do you like this story?
POLISI mkoani Kigoma imewatia mbaroni watu
watano akiwemo askari mmoja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
kwa tuhuma za kutengeneza vyeti bandia vya kitaaluma, miongoni mwake vikiwemo
90 vya uuguzi, ambavyo vilikutwa vikisubiri kugawiwa kwa wahusika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema kuwa pamoja na vyeti hivyo vya uuguzi vilivyokamatwa, pia katika operesheni hiyo walikamata vyeti 37 vya wataalamu wa maabara na vyeti tisa vya ufamasia.
Alisema kuwa katika operesheni hiyo
iliyofanywa kwa pamoja na maofisa kutoka Baraza la Wafamasia nchini, walikamata
jumla ya vyeti 936 vikiwa kwenye hatua ya ukamilishaji vikiwa bado
havijaandikwa majina, miongoni mwake vikiwemo vyeti 667 vya wauguzi wasaidizi, vyeti
126 vya wataalam wa maabara, cheti kimoja cha mafunzo ya afya ya jamii na vyeti
viwili vya utoaji huduma ya kwanza.
Katika kuhakikisha wanakuwa na uthibitisho wa
tuhuma hizo, Kamanda Mtui alisema kuwa pia wamekamata mihuri 25 ya taasisi
mbalimbali ikiwemo nyundo mbili, ambazo hutumika kutengenezea mihuri mbalimbali
ya moto.
Aliwataja watu waliokamatwa katika operesheni
hiyo ambayo inahusisha mtandao wa watu mbalimbali kuwa ni askari wa JWTZ, Mgeni
Nyamubozi ambaye ni mume wa mmiliki wa Duka la Vifaa vya Ofisi la Upendo,
lililopo Mwanga mjini Kigoma, ambalo linatuhumiwa kuhusika na utengenezaji wa
vyeti hivyo.
Katika duka hilo, Kamanda huyo wa polisi
alisema polisi walikamata kompyuta mpakato moja, ikiwa na nakala za vyeti
mbalimbali za vyuo na idara za serikali.
Mwingine aliyekamatwa ni Dickson Mshahili,
muuguzi katika Hospitali ya Mkoa Kigoma ambaye katika upekuzi nyumbani kwake,
alikutwa na nyaraka mbalimbali ikiwemo madaftari 12 yakiwa na kumbukumbu za
vyeti anavyotengeneza na mihuri ya waganga wakuu wa mikoa ya Kigoma, Kagera,
Mwanza, Singida na Tabora.
Sambamba nao alikamatwa Zawadi James, muuguzi
wa Kituo cha Afya Ujiji ambaye baada ya kupekuliwa nyumbani kwake, alikutwa na
vyeti vitatu na kabuleta ya pikipiki ambayo hutumika kutengeneza mihuri ya
moto.
Wengine waliokamatwa ni Johnson Nyabuzoka,
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlole ya mjini Kigoma, ambaye ni mtaalam wa
kompyuta aliyekuwa akitumika kufanya kazi hiyo; na Stephano Erasto ambaye
alikamatwa katika siku yake ya kwanza tangu ajiunge na duka hilo kwa ajili ya
kusaidia kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WATU WATANO AKIWEMO ASKARI WA JWTZ WATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUTENGENEZA VYETI FEKI.”
Post a Comment