Tuesday, August 16, 2016

HATIMAYE MZEE AKILIMALI AWEKA SIRAHA CHINI NA KUMUOMBA MSAMAHA MANJI.




Baada ya wanachama wa klabu ya Yanga kumfuta uanachma mzee Akilimali Katibu wa baraza la wazee Yanga, amejitokeza na kuomba radhi wanachama pamoja na mwenyekiti Yusuph Manji huku akisema yeye ni mmoja wa watu wanaompenda  sana Manji.

Akiongea na Kituo cha Radio cha EFM jijini Dar es Salaam , Mzee Akilimali wakisemwa "Hatuna tatizo na Manji tumeshamalizana na ataendelea kuwa mwenyekiti wa Yanga mpaka pale atakapo amua kuacha mwenyewe"

Akiendelea kuelezea alikiri kuwa chombo chenye maamuzi ndani ya klabu ya Yanga sio baraza la wazee ambaye yeye ni Katibu wa baraza hilo bali ni baraza la wadhamini.

Hata hivyo pamoja na Mzee Akilimali kuomba radhi bado kikao cha wenyeviti wa matawi Kwa klabu ya Yanga wamepitisha pendekezo la kumsimamisha uanachama Mzee Akilimali.

0 Responses to “HATIMAYE MZEE AKILIMALI AWEKA SIRAHA CHINI NA KUMUOMBA MSAMAHA MANJI.”

Post a Comment

More to Read