Sunday, August 14, 2016

MGOSI ASTAAFU RASMI SOKA LEO


Mgosi akiwapungia mkono mashabiki wa Simba waliofulika katika uwanja wa Taifa leo kushuhudia Mechi.

Familia ya Mgosi Pia walikuwepo Kuona kushuhudia kustaafu kwa Mgosi leo






Nahodha wa Kikosi cha Simba Mussa Hassan Mgosi leo amestaafu rasmi kuichezea klabu yake ya Simba na soka Kwa ujumla ambapo sasa anaenda kuwa meneja wa kikosi cha Simba. 

Mgosi amehitimisha safari yake ya kucheza soka leo katika mchezo wa kirafiki wa kikataifa kati ya Simba na URA ambapo vikosi hivyo vilimaliza.mchezo wao Kwa goli 1- 1.

Katika tukio hilo la kuustaafu Kwa mgosi pia aliambatana na familia yake nzimw ambao Kwa pamoja siku zote nahodha huyu mstaafu amekuwa akisifia familia yake kuwa msaada mkubwa katika mafanikio yake ndani na nje ya uwanja.

Fahari News inamtakia kila la kheri meneja mpya wa Kikosi cha Simba Mussa Mgosi katika majukumu yake mapya.

0 Responses to “ MGOSI ASTAAFU RASMI SOKA LEO”

Post a Comment

More to Read