Saturday, August 13, 2016

YANGA YAPATA USHINDI WA KWANZA BAADA YA MIAKA 18.






Hatimaye wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika (Confederation Cup) klabu ya Yanga leo imepata ushindi wa kwanza katika michuano hiyo baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya MO Bejaia kwa goli 1-0 na kuibuka na pointi tatu.

Goli pekee kwenye mchezo huo limefungwa na Amis Tambwe dakika ya nne akimalizia mpira uliotemwa na golikipa wa Bejaia Chamseddine Rahmani aliyeokoa mpira wa kichwa wa Simon Msuva.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Yanga katika hatua hiyo katika miaka ya hivi karibuni, ikumbukwe mwaka 1998 mabingwa hao wa Tanzania walifika hatua ya makundi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika lakini hawakufanikiwa kushinda mechi hata moja badala yake waliambulia sare mbili.

Matokeo ya leo yanafufua tena matumaini ya Yanga kusonga mbele lakini wakati huo ikitegemea pia matokeo ya timu nyingine. Ili Yanga ifuzu kucheza hatua ya nusu fainali, inatakiwa kushinda mechi yake ya mwisho ugenini dhidi ya TP Mazembe lakili ikiomba Mazembe iifunge Medeama kisha mchezo utakaozikutanisha MO Bejaia dhidi ya Medeama umalizike kwa sare.

0 Responses to “YANGA YAPATA USHINDI WA KWANZA BAADA YA MIAKA 18.”

Post a Comment

More to Read