Saturday, May 10, 2014
FEDHA ZA IPTL KAA LA MOTO.
Do you like this story?
Tuhuma
za ufisadi wa zaidi ya Sh200 bilioni katika akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) zinaonekana kuwa kaa la moto na jana zilitikisa Bunge na kuibua
mvutano mkali.
Hata
hivyo, suala hilo sasa limekabidhiwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili
kubaini ukweli wake.
Tuhuma
hizo ziliibuliwa juzi na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
(NCCR-Mageuzi), ambaye alisema kashfa hiyo ni zaidi ya ile ya Akaunti ya Madeni
ya Nje (EPA) ya BoT iliyotokea mwaka 2005.
Kafulila
alisema ufisadi huo unamhusisha Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gavana wa BoT na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Umeme (Tanesco).
Ingawa
Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa
Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na
AG ni Frederick Werema.
Hata
hivyo, akihitimisha hotuba ya bajeti yake na kujibu hoja mbalimbali za wabunge,
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alimwagiza CAG na Takukuru kuchunguza tuhuma hizo
ili kubaini ukweli.
“Hoja
iliyopo na inayoleta ubishani ni kuondoa pesa kutoka akaunti ya Escrow na
kuzipeleka IPTL. Tunajiuliza kama ni ufisadi, ni ufisadi wa nini wakati fedha
zile ni za IPTL?” alihoji Pinda.
Pinda
alifafanua suala hilo lilipoandikwa kwa kirefu na gazeti dada la Mwananchi (The
Citizen), CAG aliwasiliana na Katibu Mkuu wa Nishati, Gavana wa BoT na
Mkurugenzi wa Tanesco ili kupata picha ya mchakato mzima.
“Wakati
akiendelea hivyo, CAG akapata barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Nishati akimwomba
afanye uchunguzi wa kina na wakati huo huo kamati ya PAC nayo ikamwelekeza
kuchunguza jambo hilo.”
Waziri
Mkuu aliongeza kusema: “Kwa tuhuma zenyewe zilivyo, itabidi tuwahusishe
Takukuru nao wafanye kazi kwa upande wao ili kupata ukweli.
“Kwa
maelezo na mtiririko ulivyo, kinachobaki ni tuhuma zinazojitokeza ambazo upo
uwezo mkubwa wa vyombo hivi kuweza kuzibaini. Naliomba Bunge lako likubali CAG
akubali kukamilisha kazi hiyo.”
Waziri
Mkuu alisema wako viongozi wa Serikali ambao wametuhumiwa katika suala hilo
hivyo ni vyema likachunguzwa kwa uzito wake ili wale watakaobainika wamekula
rushwa washtakiwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “FEDHA ZA IPTL KAA LA MOTO.”
Post a Comment