Sunday, May 25, 2014
KIINGILIO TAIFA STARS, MALAWI NI BUKU 5 TU.
Do you like this story?
Kiingilio cha chini
cha mechi ya kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (Flames)
itakayofanyika Jumanne (Mei 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh.
5,000.
Washabiki watakaolipa
kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu
na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa
VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
Mechi hiyo itaanza
saa 11 kamili jioni ili kutoa fursa kwa washabiki wengi zaidi kuishuhudia kwa
vile itakuwa ni siku ya kazi.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili asubuhi ya siku hiyo hiyo
ya mechi kutoka Tukuyu mkoani Mbeya ambapo imepiga kambi yake chini ya Kocha
Mholanzi Mart Nooij.
Malawi (Flames)
inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Young Chidmozi tayari ipo nchini kwa
ajili ya mechi hiyo inayotumiwa na timu zote kama maandalizi ya mwisho kwa
ajili mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON).
Wakati Stars kwenye
mechi za AFCON itarudiana na Zimbabwe jijini Harare, Flames nayo itakuwa
ugenini N’djamena kukabili Chad.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIINGILIO TAIFA STARS, MALAWI NI BUKU 5 TU. ”
Post a Comment